08 – Mwanamke kutoka hali ya kujitia manukato

Miongoni mwa makosa yanayoenda kinyume na Shari´ah ni mwanamke kutoka hali ya kuwa amejipulizia manukato. Jambo hilo ni haramu, bali ni katika madhambi makubwa. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Atapojipulizia mwanamke manukato akapita karibu na watu ili wanuse harufu yake, basi huyo ni mzinzi.”[1]

[1] Abu Daawuud na at-Tirmidhiy ambaye amesema:

”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ul-Jaamiy” (01/120) nr. 323.

  • Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 28
  • Imechapishwa: 27/02/2026