23 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Tangu Malaika wa baragumu alipokabidhiwa, hajaachapo kuacha kuiangalia ´Arshi kwa kuchelea asije kuamrishwa kabla ya kumaliza kupepesa macho. Macho yake yanang´aa kana kwamba ni mng´ao wa nyota mbili[1].”[2]

Ameipokea al-Haakim ambaye ameisahihisha[3].

[1] Hajapatapo kuyafunga hata dakika moja akichunga na kusubiri amri ya Allaah.

[2] al-Haakim (04/559) ambaye amesema:

”Cheni ya wapokezi wa Hadiyth ni Swahiyh.”

[3] Mtunzi ameafikiana naye katika “Talkhiysw-ul-Mustadrak” (4/55) na akaitilia nguvu zaidi kwa mujibu wa sharti za Muslim. Mambo ni kama alivosema. Abush-Shaykh pia ameipokea katika “al-´Adhwamah”  (01/73) na akaitajia yenye kuitilia nguvu kutoka katika Hadiyth ya Ibn ´Abbaas.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 93
  • Imechapishwa: 24/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy 23. Kitabu kilichoko kwa Allaah juu ya ´Arshi

    21 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

    “Wakati Allaah (´Azza wa Jall) alipohukumu viumbe aliandika katika kitabu Chake kilichoko Kwake juu ya ´Arshi: ”Hakika huruma Yangu inashinda ghadhabu Zangu.”[1]

    Imekuja Katika tamko jengine:

    “Allaah kabla hajaumba viumbe aliandika kitabu: “Hakika huruma Yangu inashinda ghadhabu Zangu.” Kiko Kwake juu ya ´Arshi.”

    Imekuja Katika tamko jengine:

    ”Wakati Allaah alipoumba viumbe, aliandika kitabu juu yake Mwenyewe. Kimenyanyuliwa juu ya ´Arshi: “Hakika huruma Yangu inashinda ghadhabu Zangu.”[2]

    [1] al-Bukhaariy (3194), Muslim (2751), Ahmad (2/466) na wengineo.

    [2] Hadiyth ni Swahiyh. Baadhi ya matamshi yake yapo kwa al-Bukhaariy na Muslim. Tamko la mwisho liko kwa at-Tirmidhiy. Nimeitaja katika “as-Swahiyhah” (1629) na ”Dhwilaal-ul-Jannah fiy Takhriyj-is-Sunnah” (810-811).

    Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
    Mfasiri: Firqatunnajia.com
    Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 92
    Imechapishwa: 12/04/2024
    taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy

    https://firqatunnajia.com/23-kitabu-kilichoko-kwa-allaah-juu-ya-arshi/