Mpaka hapa mada muhimu niliokuwa nataka kuizungumzia na ambayo watu wengi wamepewa mtihani kwayo imeisha.

Mlango wa tawbah bado umefunguliwa kwa yule anayetaka kutubia. Ndugu yangu muislamu! Hakikisha umekimbilia kutubu haraka iwezekanavyo na umtakasie ´ibaadah Allaah (´Azza wa Jall), yajutie yale yaliyopita, uazimie kutorudi tena na ukithirishe matendo mema mengi:

إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ يُبَدِّلُ اللَّـهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا وَمَن تَابَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَإِنَّهُ يَتُوبُ إِلَى اللَّـهِ مَتَابًا

“Isipokuwa [hatoadhibiwa] yule aliyetubu na akaamini na akatenda matendo mema. Hao Allaah atawabadilishia maovu yao kuwa mema, [kwa sababu] Allaah daima ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu; na atakayetubu na akatenda mema, basi hakika yeye ametubia kwa Allaah tawbah ya kweli.”[1]

Ninamuomba Allaah (Ta´ala) atuonyeshe njia iliyonyooka na atuongoze sote katika njia Yake iliyonyooka ambayo amewaneemesha nayo – Mitume na wakweli na mashahidi na waja wenye kutenda mema; na sio ya wale walioghadhibikiwa na wakapotea!

Imeandikwa na mja fakiri wa Allaah (Ta´ala) Muhammad bin Swaalih al-´Uthaymiyn

407-02-23

[1] 25:70-71

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Hukm Taarik-is-Swalaah, uk. 23
  • Imechapishwa: 22/10/2016