Nubayshah al-Hudhaliy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Siku za Tashriyq ni siku za kula na kunywa.”
Imekuja katika upokezi mwingine:
”… na kumtaja Allaah (´Azza wa Jall).”[1]
Ameipokea Muslim.
Hadiyth hii ni dalili juu ya fadhilah ya siku za Tashriyq, nazo ni siku ya 11, 12 na 13. Zimeitwa hivyo kwa sababu watu walikuwa wanaanika kuelekea mashariki nyama za Udhhiyah na Hadiy. Kwa msemo mwingine wanazikausha kwa kukata vipande na kuzianika ili zikauke. Nazo ni miongoni mwa siku zenye fadhilah na misimu mikuu, nazo ndizo siku zilizohesabiwa zilizotajwa katika maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):
وَاذْكُرُوا اللَّـهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ
“Na mtajeni Allaah katika siku za kuhesabika.”[2]
Hakuna ambaye ameona kinyume, kama walivyonukuu wengi.
[1] Muslim (1141).
[2] 02:203
- Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 40-41
- Imechapishwa: 15/05/2025
Nubayshah al-Hudhaliy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Siku za Tashriyq ni siku za kula na kunywa.”
Imekuja katika upokezi mwingine:
”… na kumtaja Allaah (´Azza wa Jall).”[1]
Ameipokea Muslim.
Hadiyth hii ni dalili juu ya fadhilah ya siku za Tashriyq, nazo ni siku ya 11, 12 na 13. Zimeitwa hivyo kwa sababu watu walikuwa wanaanika kuelekea mashariki nyama za Udhhiyah na Hadiy. Kwa msemo mwingine wanazikausha kwa kukata vipande na kuzianika ili zikauke. Nazo ni miongoni mwa siku zenye fadhilah na misimu mikuu, nazo ndizo siku zilizohesabiwa zilizotajwa katika maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):
وَاذْكُرُوا اللَّـهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ
“Na mtajeni Allaah katika siku za kuhesabika.”[2]
Hakuna ambaye ameona kinyume, kama walivyonukuu wengi.
[1] Muslim (1141).
[2] 02:203
Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 40-41
Imechapishwa: 15/05/2025
https://firqatunnajia.com/24-hadiyth-siku-za-tashriyq-ni-siku-za-kula-na-kunywa/