الْحَمْدُ لِلَّه وَحْدَهُ وَالصًّلاَةُ وَالسَّلاَمُ عَلَى مَنْ لاَ نَبَيِّ بَعْدَهُ
”Himdi zote anastahiki Allaah pekee, swalah na salamu ziwe juu ya yule ambaye hakuna Nabii mwengine baada yake.”[1]
75-
أَعُوذُ بِاللّهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ
اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ
”Najilinda kwa Allaah, kutokamana na shaytwaan aliyefukuzwa mbali. Allaah, hapana mungu wa haki mwingine isipokuwa Yeye, aliyehai daima, msimamia kila kitu. Haumchukui usingizi wala kulala. Ni Vyake pekee vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Nani huyu ambaye anashufai mbele Yake bila ya idhini Yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawawezi kuzunguka chochote katika ujuzi Wake isipokuwa kwa alitakalo. Kursiy Yake imeenea mbingu na ardhi wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo – Naye ni yujuu kabisa, ametukuka kabisa.”[2]
76-
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم. قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ اللَّـهُ الصَّمَدُ لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ
”Kwa jina la Allaah, Mwingi wa kurehemu, Mwenye kurehemu. Sema: ”Allaah ni Mmoja pekee, Mwenye kutegemewa kwa haja zote, hakuzaa na wala hakuzaliwa na wala haiwi awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye.”[3]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ .قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَق مِن شَرِّ مَا خَلَقَ وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ وَمِن شَرِّ النَّفَّاثَاتِ فِي الْعُقَدِ وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ
”Kwa jina la Allaah, Mwingi wa kurehemu, Mwenye kurehemu. Sema: ”Najilinda na Mola wa mapambazuko, kutokamana na shari ya alivyoviumba, na kutokamana na shari ya giza linapoingia, kutokamana na shari ya wapulizao mafundoni na kutokamana na shari ya hasidi anapohusudu.”[4]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ .قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ مَلِكِ النَّاسِ إِلَـٰهِ النَّاسِ مِن شَرِّ الْوَسْوَاسِ الْخَنَّاسِ الَّذِي يُوَسْوِسُ فِي صُدُورِ النَّاسِ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ
”Kwa jina la Allaah, Mwingi wa kurehemu, Mwenye kurehemu. Sema: ”Najilinda na Mola wa watu, mfalme wa watu, mwabudiwa wa haki wa watu, kutokamana na shari za anayetia wasiwasi, mwenye kurejea nyuma, anayetia wasiwasi nyoyoni mwa watu miongoni mwa majini na watu.”[5]
Kila moja mara 3[6].
77-
أَصْـبَحْنا وَأَصْـبَحَ المـلكُ لله وَالحَمدُ لله، لا إلهَ إلاّ اللّهُ وَحدَهُ لا شَريكَ لهُ، لهُ المُـلكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كلّ شَيءٍ قدير، رَبِّ أسْـأَلُـكَ خَـيرَ ما في هَذا الْيَوْمِ وَخَـيرَ ما بَعْـدَهُ، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْ شَـرِّ هَذا الْيَوْمِ وَشَرِّ ما بَعْـدَهُ، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنَ الْكَسَـلِ وَسـوءِ الْكِـبَر، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنْ عَـذابٍ في النّـارِ وَعَـذابٍ في القَـبْر
”Tumepambaukiwa na umekuwa ufalme ni wa Allaah, himdi zote ni stahiki ya Allaah, hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee, hana mshirika. Ni Wake ufalme, na ni Zake himdi zote njema, Naye juu ya kila jambo ni muweza. Mola wa wangu, nakuomba kheri ya siku ya leo, kheri ya baada yake, na najilinda Kwako kutokamana na shari ya siku ya leo na shari ya baada yake. Mola wangu, najilinda Kwako kutokamana na uvivu na uzee mbaya. Mola wangu, najilinda Kwako kutokamana na adhabu ya Moto na adhabu ya kaburi.”
Itapoingia jioni utasema:
أَمْسَيْـنا وَأَمْسـى المـلكُ لله وَالحَمدُ لله، لا إلهَ إلاّ اللّهُ وَحدَهُ لا شَريكَ لهُ، لهُ المُـلكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كلّ شَيءٍ قدير، رَبِّ أسْـأَلُـكَ خَـيرَ ما في هـذهِ اللَّـيْلَةِ وَخَـيرَ ما بَعْـدَهـا، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْ شَـرِّ هـذهِ اللَّـيْلةِ وَشَرِّ ما بَعْـدَهـا، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنَ الْكَسَـلِ وَسـوءِ الْكِـبَر، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنْ عَـذابٍ في النّـارِ وَعَـذابٍ في القَـبْر
”Tumeingiliwa na jioni na umekuwa ufalme ni wa Allaah, himdi zote ni stahiki ya Allaah, hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee, hana mshirika. Ni Wake ufalme, na ni Zake himdi zote njema, Naye juu ya kila jambo ni muweza. Mola wa wangu, nakuomba kheri ya usiku wa leo, na kheri ya baada yake, na najilinda Kwako kutokamana na shari ya usiku wa leo na shari ya baada yake. Mola wangu, najilinda Kwako kutokamana na uvivu, na uzee mbaya. Mola wangu, najilinda Kwako kutokamana na adhabu ya Moto na adhabu ya kaburi.”[7]
78-
اللّهُـمَّ بِكَ أَصْـبَحْنا وَبِكَ أَمْسَـينا، وَبِكَ نَحْـيا وَبِكَ نَمـوتُ وَإِلَـيْكَ النِّـشور
”Ee Allaah! Kwako tumepambaukiwa, na Kwako tumeingiliwa na jioni, na kwa ajili Yako ndio tumekuwa hai, na kwa ajili Yako tutakufa na Kwako tutakusanywa.”
Itapoingia jioni utasema:
اللّهُـمَّ بِكَ أَمْسَـينا، وَبِكَ أَصْـبَحْنا، وَبِكَ نَحْـيا، وَبِكَ نَمـوتُ وَإِلَـيْكَ المَصـير
”Ee Allaah! Kwako tumeingiliwa na jioni, na Kwako tumepambaukiwa, na kwa ajili Yako ndio tumekuwa hai, na kwa ajili Yako tutakufa na Kwako tutakusanywa.”[8]
79-
اللّهـمَّ أَنْتَ رَبِّـي لا إلهَ إلاّ أَنْتَ، خَلَقْتَنـي وَأَنا عَبْـدُك، وَأَنا عَلـى عَهْـدِكَ وَوَعْـدِكَ ما اسْتَـطَعْـت، أَعـوذُبِكَ مِنْ شَـرِّ ما صَنَـعْت، أَبـوءُ لَـكَ بِنِعْـمَتِـكَ عَلَـيَّ وَأَبـوءُ بِذَنْـبي فَاغْفـِرْ لي فَإِنَّـهُ لا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إِلاّ أَنْتَ
”Ee Allaah! Wewe ni Mola wangu, hapana mungu wa haki mwingine isipokuwa Wewe, umeniumba mimi na mimi ni mja Wako, nami niko juu ya ahadi Yako, na agano Lako kiasi cha niwezavyo, najilinda Kwako kutokamana na shari ya nilichokifanya, nakiri Kwako kwa kunineemesha, na nakiri kwa dhambi zangu, basi nakuomba unisamehe kwani hakuna mwengine anayesamehe dhambi isipokuwa Wewe.”[9]
80-
اللّهُـمَّ إِنِّـي أَصْبَـحْتُ أَشْـهِدُك، وَأُشْـهِدُ حَمَلَـةَ عَـرْشِـك، وَمَلائِكَتِك، وَجَمـيعَ خَلْـقِك، أَنَّـكَ أَنْـتَ اللهُ لا إلهَ إلاّ أَنْـتَ وَحْـدَكَ لا شَريكَ لَـك، وَأَنَّ ُ مُحَمّـداً عَبْـدُكَ وَرَسـولُـك
”Ee Allaah! Hakika mimi nimeamka asubuhi; ninakushuhudisha na ninawashuhudia wabeba wa ‘Arshi yako na Malaika Wako, viumbe wako wote, ya kwamba Wewe ni Allaah, hapana mungu wa haki isipokuwa Wewe, hali ya kuwa upekee yako huna mshirika, na kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wako.”
Mara 4.
Itapoingia jioni utasema:
اللّهُـمَّ إِنِّـي أَمْسَيْتُ أَشْـهِدُك، وَأُشْـهِدُ حَمَلَـةَ عَـرْشِـك، وَمَلائِكَتِك، وَجَمـيعَ خَلْـقِك، أَنَّـكَ أَنْـتَ اللهُ لا إلهَ إلاّ أَنْـتَ وَحْـدَكَ لا شَريكَ لَـك، وَأَنَّ ُ مُحَمّـداً عَبْـدُكَ وَرَسـولُـك
”Ee Allaah! Hakika mimi nimefika jioni; ninakushuhudisha na ninawashuhudia wabeba wa ‘Arshi yako na Malaika Wako, viumbe wako wote, ya kwamba Wewe ni Allaah, hapana mungu wa haki isipokuwa Wewe, hali ya kuwa upekee yako huna mshirika, na kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wako.”
Mara 4[10].
81-
اللّهُـمَّ ما أَصْبَـَحَ بي مِـنْ نِعْـمَةٍ أَو بِأَحَـدٍ مِـنْ خَلْـقِك، فَمِـنْكَ وَحْـدَكَ لا شريكَ لَـك، فَلَـكَ الْحَمْـدُ وَلَـكَ الشُّكْـر
”Ee Allaah! Sikuamka na neema yoyote au kutoka kwa kiumbe Chako chochote, si vyenginevyo isipokuwa inatoka Kwako, hali ya kuwa upekee huna mshirika, ni Zako himdi zote njema na ni Zako shukurani.”
Itapoingia jioni utasema:
اللّهُـمَّ ما أَمْسَى بِي مِـنْ نِعْـمَةٍ أَو بِأَحَـدٍ مِـنْ خَلْـقِك، فَمِـنْكَ وَحْـدَكَ لا شريكَ لَـك، فَلَـكَ الْحَمْـدُ وَلَـكَ الشُّكْـر
”Ee Allaah! Sikufikiwa jioni na neema yoyote au kutoka kwa kiumbe Chako chochote, si vyenginevyo isipokuwa inatoka Kwako, hali ya kuwa upekee huna mshirika, ni Zako himdi zote njema na ni Zako shukurani.”[11]
82-
اللّهُـمَّ عافِـني في بَدَنـي، اللّهُـمَّ عافِـني في سَمْـعي، اللّهُـمَّ عافِـني في بَصَـري، لا إلهَ إلاّ أَنْـتَ. اللّهُـمَّ إِنّـي أَعـوذُبِكَ مِنَ الْكُـفر، وَالفَـقْر، وَأَعـوذُبِكَ مِنْ عَذابِ القَـبْر، لا إلهَ إلاّ أَنْـتَ
”Ee Allaah! Nipe afya katika mwili wangu. Ee Allaah! Nipe afya katika usikizi wangu. Ee Allaah! Nipe afya katika uoni wangu. Hapana mungu wa haki isipokuwa Wewe. Ee Allaah! Hakika mimi najilinda Kwako kutokamana na ukafiri, ufakiri na najilinda Kwako kutokamana na adhabu ya kaburi. Hapana mungu wa haki isipokuwa Wewe.”
Mara 3[12].
83-
حَسْبِـيَ اللّهُ لا إلهَ إلاّ هُوَ عَلَـيهِ تَوَكَّـلتُ وَهُوَ رَبُّ العَرْشِ العَظـيم
”Ananitosheleza Allaah, hapana mungu wa haki mwengine isipokuwa Yeye, Kwake Yeye ni mwenye kutegemea na Yeye ni Mola wa ´Arshi tukufu.”
Mara 7 asubuhi na jioni[13].
84-
اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ العَـفْوَ وَالعـافِـيةَ في الدُّنْـيا وَالآخِـرَة، اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ العَـفْوَ وَالعـافِـيةَ في ديني وَدُنْـيايَ وَأهْـلي وَمالـي، اللّهُـمَّ اسْتُـرْ عـوْراتي وَآمِـنْ رَوْعاتـي، اللّهُـمَّ احْفَظْـني مِن بَـينِ يَدَيَّ وَمِن خَلْفـي وَعَن يَمـيني وَعَن شِمـالي، وَمِن فَوْقـي، وَأَعـوذُ بِعَظَمَـتِكَ أَن أُغْـتالَ مِن تَحْتـي
”Ee Allaah! Hakika nakuomba msamaha na unisalimishe duniani na Aakhirah. Ee Allaah! Hakika nakuomba msamaha na unisalimishe katika dini na dunia yangu, familia yangu na mali yangu. Ee Allaah! Nisitiri uchi wangu na iaminishe khofu yangu. Ee Allaah! Nihifadhi mbele yangu, nyuma yangu, kuliani mwangu, kushotoni mwangu, juu yangu na najilinda kwa utukufu Wako kuuliwa chini yangu.”[14]
85-
اللّهُـمَّ عالِـمَ الغَـيْبِ وَالشّـهادَةِ فاطِـرَ السّماواتِ وَالأرْضِ رَبَّ كـلِّ شَـيءٍ وَمَليـكَه، أَشْهَـدُ أَنْ لا إِلـهَ إِلاّ أَنْت، أَعـوذُ بِكَ مِن شَـرِّ نَفْسـي وَمِن شَـرِّ الشَّيْـطانِ وَشِـرْكِه، وَأَنْ أَقْتَـرِفَ عَلـى نَفْسـي سوءاً أَوْ أَجُـرَّهُ إِلـى مُسْـلِم
”Ee Allaah! Mjuzi wa yaliyojificha na yenye kuonekana, Mwanzishi wa mbingu na ardhi, Mola wa kila kitu na Mwenye kukimiliki. Nashuhudia kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Wewe. Najilinda Kwako kutokamana na shari ya nafsi yangu na shari ya shaytwaan na shirki yake na kujichumia uovu juu ya nafsi yangu au kumletea nao muislamu.”[15]
86-
بِسـمِ اللهِ الذي لا يَضُـرُّ مَعَ اسمِـهِ شَيءٌ في الأرْضِ وَلا في السّمـاءِ وَهـوَ السّمـيعُ العَلـيم
”Kwa jina la Allaah ambaye hakidhuru kwa jina Lake chochote kilichoko ardhini wala mbinguni; Naye ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa kila kitu.”
Mara 3[16].
87-
رَضيـتُ بِاللهِ رَبَّـاً وَبِالإسْلامِ ديـناً وَبِمُحَـمَّدٍ صَلى الله عليه وسلم نَبِيّـاً
”Nimeridhia Allaah kuwa ndiye Mola wangu, Uislamu kuwa ndio dini yangu na Muhammad kuwa ndiye Mtume wangu.”
Mara 3[17].
88-
يا حَـيُّ يا قَيّـومُ بِـرَحْمَـتِكِ أَسْتَـغـيث، أَصْلِـحْ لي شَـأْنـي كُلَّـه، وَلا تَكِلـني إِلى نَفْـسي طَـرْفَةَ عَـين
”Ee Uliyehai daima, Mwenye kukisimamia kila kitu, kwa rehema Zako naomba uokozi, nitengenezee mambo yangu yote na wala usiniegemezee mambo yangu mwenyewe [pasi na msaada wako] hata kwa muda wa kupepesa jicho.”[18]
89-
أَصْبَـحْـنا وَأَصْبَـحْ المُـلكُ للهِ رَبِّ العـالَمـين، اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ خَـيْرَ هـذا الـيَوْم، فَـتْحَهُ، وَنَصْـرَهُ، وَنـورَهُ وَبَـرَكَتَـهُ، وَهُـداهُ، وَأَعـوذُ بِـكَ مِـنْ شَـرِّ ما فـيهِ وَشَـرِّ ما بَعْـدَه
”Tumepambaukiwa na umekuwa ufalme ni wa Allaah na ufalme ni wa Allaah, Mola wa walimwengu. Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba kheri ya siku hii ya leo, ufunguzi wake, nusura yake, nuru yake, baraka yake, uongofu wake na najilinda Kwako kutokamana na shari ya kilicho ndani ya siku yake na shari ya baada yake.”
Itapoingia jioni utasema:
أَمْسَيْـنا وَأَمْسـى المُـلكُ للهِ رَبِّ العـالَمـين، اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ خَـيْرَ هـذهِ اللَّـيْلَة، فَتْحَهـا، وَنَصْـرَهـا، وَنـورَهـا، وَبَـرَكَتَـهـا، وَهُـداهـا، وَأَعـوذُ بِـكَ مِـنْ شَـرِّ ما فـيهـاِ وَشَـرِّ ما بَعْـدَهـا
”Tumeingiliwa na jioni na umekuwa ufalme ni wa Allaah na ufalme ni wa Allaah, Mola wa walimwengu. Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba kheri ya siku hii ya leo, ufunguzi wake, nusura yake, nuru yake, baraka yake, uongofu wake na najilinda Kwako kutokamana na shari ya kilicho ndani ya siku yake na shari ya baada yake.”[19]
90-
أَصْـبَحْنا علـى فِطْـرَةِ الإسْلام، وَعَلـى كَلِـمَةِ الإخْـلاص، وَعلـى دينِ نَبِـيِّنا مُحَـمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم وَعَاـى مِلَّـةِ أبينـا إِبْـراهيـمَ حَنيـفاً مُسْلِـماً وَمـا كـانَ مِنَ المُشـرِكيـن
”Tumepambaukiwa tukiwa juu ya maumbile ya Uislamu, juu ya neno la ikhlaasw, juu ya dini ya Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), juu ya mila ya baba yetu Ibraahiym, aliyejiepusha na shirki aina zote na akaielekea Tawhiyd, hali ya kuwa muislamu wala hakuwa miongoni mwa washirikina.”
Itapoingia jioni utasema:
أَمْسَيْنا علـى فِطْـرَةِ الإسْلام، وَعَلـى كَلِـمَةِ الإخْـلاص، وَعلـى دينِ نَبِـيِّنا مُحَـمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم وَعَاـى مِلَّـةِ أبينـا إِبْـراهيـمَ حَنيـفاً مُسْلِـماً وَمـا كـانَ مِنَ المُشـرِكيـن
”Tumeingiliwa na jioni tukiwa juu ya maumbile ya Uislamu, juu ya neno la ikhlaasw, juu ya dini ya Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), juu ya mila ya baba yetu Ibraahiym, aliyejiepusha na shirki aina zote na akaielekea Tawhiyd, hali ya kuwa muislamu wala hakuwa miongoni mwa washirikina.”[20]
91-
سُبْحـانَ اللهِ وَبِحَمْـدِهِ
”Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu yote na himdi zote njema ni Zake.”
Mara 100[21].
92-
لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ لا شَـريكَ لهُ، لهُ المُـلْكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كُلّ شَيءٍ قَدير
”Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, ni Wake ufalme na ni Zake himdi zote njema, Naye juu ya kila jambo ni muweza.”
Mara 10[22] au mara 1 ukihisi uvivu[23].
93-
لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ لا شَـريكَ لهُ، لهُ المُـلْكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كُلّ شَيءٍ قَدير
”Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, ni Wake ufalme na ni Zake himdi zote njema, Naye juu ya kila jambo ni muweza.”
Mara 100 utapoamka asubuhi[24].
94-
سُبْحـانَ اللهِ وَبِحَمْـدِهِ عَدَدَ خَلْـقِه، وَرِضـا نَفْسِـه، وَزِنَـةَ عَـرْشِـه، وَمِـدادَ كَلِمـاتِـه
”Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu yote na himdi zote njema ni Zake kwa idadi ya viumbe Wake, radhi Yake, uzito wa ´Arshi Yake na wino wa maneno Yake.”
Mara 3 utapoamka asubuhi[25].
95-
اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْأَلُـكَ عِلْمـاً نافِعـاً وَرِزْقـاً طَيِّـباً، وَعَمَـلاً مُتَقَـبَّلاً
”Ee Allaah! Hakika nakuomba elimu yenye kunufaisha, riziki njema na matendo yenye kukubaliwa.”
Atasema haya akiamka asubuhi[26].
96-
أَسْتَغْفِرُ الَّلهَ وَ أَتُوبُ إِلَيْهِ
”Namuomba Allaah msamaha na natubu Kwake.”
Mara 100 kwa kila siku[27].
97-
أَعُوْذُ بِكَلِماتِ اللَّهِ التَّامَّتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ
”Najilinda kwa maneno ya Allaah yaliyotimia kutokamana na shari Alivyoviumba.”
Mara 3 akiingiliwa na jioni[28].
98-
اللّهُـمَّ صَلِّ عَلـى مُحمَّـدٍ وَعَلـى أَزْواجِـهِ وَذُرِّيَّـتِه، كَمـا صَلَّيْـتَ عَلـى آلِ إبْراهـيم. وَبارِكْ عَلـى مُحمَّـدٍ وَعَلـى أَزْواجِـهِ وَذُرِّيَّـتِه، كَمـا بارِكْتَ عَلـى آلِ إبْراهـيم. إِنَّكَ حَمـيدٌ مَجـيد
!Ee Allaah! Msifu Muhammad, wakeze na kizazi chake, kama Ulivyowasifu jamaa zake Ibraahiym. Mbariki Muhammad, wakeze na kizazi chake kama Ulivyowabariki jamaa zake Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa.”
Mara 10[29].
[1] Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Kukaa pamoja na watu wanaomdhukuru Allaah (Ta´ala) kuanzia swalah ya Fajr mpaka kuchomoza jua kunapendeza zaidi kwangu kuliko kuacha huru watu wanne miongoni mwa wana wa Ismaa’iyl. Na kukaa pamoja na watu wanaomdhukuru Allaah kuanzia swalah ya ´Aswr mpaka kuzama jua kunapendeza zaidi kwangu mimi kuliko kuwaacha huru watu wanne.”
Abu Dawuud (3667) na ni nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Abiy Daawuud (02/698).
[2] 02:255 ”Atakayeisoma kunapoingia asubuhi itamlinda na majini mpaka itakapofika jioni. Na atakayeisoma kunapoingia jioni atalindwa na majini mpaka asubuhi.” al-Haakim (01/562) na ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (01/273). Ameiegemeza kwa an-Nasaa´iy na at-Twabaraaniy ambapo akasema:
”Cheni ya wapokezi ya at-Twabaraaniy ni nzuri.”
[3] 112:01-04
[4] 113:01-05
[5] 114:01-06
[6] ”Atakayezisoma mara tatu kunapoingia asubuhi na jioni, basi zitamtosheleza kutokamana na kila shari.” Abu Daawuuud (04/322), at-Tirmidhiy (05/567). Tazama ”Swahiyh-ut-Tirmidhiy”(03/182).
[7] Muslim (04/2088).
[8] at-Tirmidhiy (05/466). Tazama ”Swahiyh-ut-Tirmidhiy” (03/142).
[9] ”Atakayeyasema mchana hali ya kuwa na yakini nayo ambapo akafariki siku hiyo kabla kuingia jioni, basi ataingia Peponi. Atakayeyasema usiku hali ya kuwa na yakini nayo ambapo akafariki siku hiyo kabla kuingia asubuhi, basi ataingia Peponi.” al-Bukhaariy (07/150).
[10] ”Atakayeyasema haya mara nne pindi anapoamka asubuhi au imapoingia jioni, basi Allaah atamuepusha na Moto.” Abu Daawuud (04/317), al-Bukhaariy katika ”Aadab-ul-Mufrad (1201), an-Nasaa´iy katika ”‘Amal-ul-Yawm wal-Laylah (09), Ibn-us-Sunniy (70). Shaykh Ibn Baaz ameifanya cheni ya wapokezi ya an-Nasaa´iy na Abu Daawuud kuwa nzuri katika ”Tuhfat-ul-Akhyaar”, uk. 23.
[11] ”Atakayeyasema pindi anapoamka asubuhi, basi hakika ametekeleza shukurani ya siku yake. Na atakayesema inapoingia jioni, basi ametekeleza shukurani ya usiku wake.” Abu Daawuud (04/318), an-Nasaa´iy katika “‘Amal-ul-Yawm wal-Laylah (07), Ibn-us-Sunniy (41), Ibn Hibbaan katika “Mawaarid” (2361) Ibn Baaz ameifanya cheni ya wapokezi kuwa nzuri katika ”Tuhfat-ul-Akhyaar”, uk. 24.
[12] Abu Daawuud (04/324), Ahmad (05/42), an-Nasaa´iy katika ”‘Amal-ul-Yawm wal-Laylah (22), Ibn-us-Sunniy (69) na al-Bukhaariy katika ”Aadab-ul-Mufrad”. ´Allaamah Ibn Baaz ameifanya cheni ya wapokezi kuwa nzuri katika “Tuhfat-ul-Akhyaaar”, uk. 26.
[13] ”Atakayeyasema mara saba pindi kunapopambazuka na kunapoinga jioni, basi itamtosheleza katika mambo yake yanayomtia hamu ya dunia na Aakhirah.” Ibn-us-Sunniy (71) kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Abu Daawuud (04/321) kutoka kwa Swahabah. Shu’ayb na ‘Abdul-Qaadir al-Arnauutw wameisahihisha cheni ya wapokezi wake. Tazama ”Zaad-ul-Ma’aad (02/376) .
[14] Abu Daawuud (5074) na Ibn Maajah (3871). Tazama ”Swahiyh Ibn Maajah (02/332).
[15] at-Tirmidhiy (3392) na Abu Daawuud (5067). Swahiyh-ut-Tirmidhiy (03/142).
[16] “Atakayeyasema mara tatu kunapoingia asubuhi na jioni, basi hatodhuriwa na chochote.” Abu Daawuud (04/323), at-Tirmidhiy (05/465), Ibn Maajah (3869) na Ahmad. Tazama “Swahiyh Ibn Maajah (02/332). ‘Allaamah Ibn Baaz ameifanya cheni ya wapokezi wake kuwa nzuri katika “Tuhfat-ul-Akhyaar”, uk. 39.
[17] “Atakayeyasema mara tatu kutapoingia asubuhi na mara tatu kutapoingia jioni, basi imekuwa ni haki kwa Allaah kumridhia siku ya Qiyaamah.” Ahmad (04/337), an-Nasaa´iy katika “‘Amal-ul-Yawm wal-Laylah” (04), Ibn-us-Sunniy (68), Abu Daawuud (04/318) na at-Tirmidhiy (05/465). Ibn Baaz ameifanya kuwa nzuri katika “Tuhfat-ul-Akhyaa, uk. 39.
[18] al-Haakim na ameisahihisha ambapo adh-Dhahabiy akaafikiana naye. Tazama ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (01/273).
[19] Abu Daawuud (04/322). Shu’ayb na ‘Abdul-Qaadir al-Arnauutw wameifanya cheni ya wapokezi wake kuwa nzuri wakati wa kuihakiki ”Zaad-ul-Ma’aad (02/273).
[20] Ahmad (03/406, 407) na Ibn-us-Sunny katika ”‘Amal-ul-Yawm wal-Laylah (34). Tazama ”Swahiyh-ul-Jaamiy’” (04/209).
[21] ”Atakayeyasema mara mia kunapopambazuka na kunapoingia jioni, basi hakuna yeyote siku ya Qiyaamah atakayekuja na kitu bora kuliko alichokuja nacho yeye isipokuwa aliyesema mfano wa haya au akazidisha.” Muslim (04/2071).
[22] an-Nasaa´y katika ”‘Amal-ul-Yawm wal-Laylah” (24). Tazama ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (01/272) na ”Tuhfat-ul-Akhyaar”, uk. 255 ya Ibn Baaz. Pia tazama fadhilah zake katika ukurasa wa 146 Hadiyth nambari. 255.
[23] Abu Daawuud (04/319), Ibn Maajah (3867) na Ahmad (04/60). Tazama ”Swahiyh ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (01/270) na ”Swahiyh Abiy Daawuud” (03/957).
[24] ”Atakayeyasema mara kumi kwa siku, basi ataandikiwa thawabu sawa na kuacha huru watumwa kumi, ataandikiwa mema mia moja, atafutiwa makosa mia moja moja, atakuwa na kinga dhidi ya shaytwaan kwa siku hiyo hadi kuingie jioni na hakuna atakayekuja na kitu bora kuliko alichokuja nacho yeye isipokuwa tu yule aliyefanya zaidi ya hivo.” al-Bukhaariy (04/95) na Muslim (04/2071).
[25] Muslim (04/2090).
[26] Ibn-us-Sunniy katika ”‘Amal-ul-Yawam wal-Laylah” (54), Ibn Maajah (925). ´Abdul-Qaadir al-Arnauutw na Shu´ayb wameifanya nzuri cheni ya wapokezi wake wakati wa kuihakiki ”Zaad-ul-Ma´aad” (0/375). Imekwishatangulia katika uk. 51 nambari (73).
[27] al-Bukhaariy pamoja na al-Fath (11/101) na Muslim (4/2075).
[28] “Atakayeyasema mara tatu jioni, basi hatodhuriwa na mdudu wa sumu usiku huo.” Ahmad (02/290), an-Nasaa´iy katika “‘Amal-ul-Yawm wal-Laylah” (590) na Ibn-us-Sunniy (68). Tazama “Swahiyh-ut-Tirmidhiy (03/187), “Swahiyh Ibn Maajah” (92/266), “Tuhfat-ul-Akhyaar”, uk. 45.
[29] “Atakayeniswalia mara kumi kunapoingia asubuhi na mara kumi kunapoingia jioni, basi nitamuombea uombezi siku ya Qiyaamah.” Ameipokea at-Twabaraaniy kwa cheni mbili ambapo moja katika hizo mbili ni nzuri. Tazama “Majma´-uz-Zawaa-id” (10/120) na ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (01/273).
- Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Huswn-ul-Muslim
- Imechapishwa: 27/04/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)