Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Wako kati na kati baina ya Murji-ah wanaosema kuwa imani haidhuriki kitu kwa maasi. Wanaona kuwa imani ya mtu haidhuriki kwa madhambi yake muda wa kuwa anaamini ndani ya moyo wake. Watu hawa wamejiaminisha na vitimbi ya Allaah. Hawayaingizi matendo ndani ya imani na kwa ajili hiyo wanaona kuwa mtu ataingia Peponi hata kama hakufanya chochote. ´Aqiydah hii imeharibu ulimwengu. Matokeo yake watu wameivunja dini kutokana na fikira hiyo. Fikira yao wameona kuwa midhali wataingia Peponi basi hawana haja ya kufanya matendo. Matokeo yake wanafanya wayatakayo.
Na wako kati na kati baina ya Khawaarij ambao wanakufurisha kwa madhambi makubwa yaliyo chini ya shirki. Wanaona kutekeleza maandiko yote ya matishio juu ya watenda madhambi. Ni kweli kwamba amewatishia watenda madhambi, lakini pia amesema:
إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ
“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae.”[1]
Allaah ndiye atakayeamua cha kuwafanya.
Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah – iko na kati. Haki iko pamoja na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, ambao wako wako na kati baina ya usalama na matarajio, na khofu na kukata tamaa. Kwa ajili hiyo wanaona kuwa khofu na matarajio kwa nisba ya mtu inatakiwa iwe kama mbawa za ndege; ikiwa mbawa yake moja itaingia kasoro, basi ndege anaanguka. Vivyo hivyo mwanadamu; ikiwa khofu au matarajio yake yataingia kasoro, basi anaanguka. Ni lazima kusawazisha kama zinavyosawazishwa mabawa ya ndege.
[1]4:48
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 262
- Imechapishwa: 21/05/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket