Miongoni mwa ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kuwa kati na kati baina ya kujiaminisha na vitimbi vya Allaah na kukata tamaa na rehema Zake. Wanataraji rehema za Allaah lakin hawahisi salama kutokana na vitimbi, adhabu na mtihani wa Allaah. Sambamba na hayo hawakati tamaa na rehema za Allaah. Kwa msemo mwingine wanakusanya kati ya kuwa na khofu na matarajio, kama walivokuwa wakifanya Mitume. Allaah (Subhaanah) amesema kuhusu Mitume:
إِنَّهُمْ كَانُوا يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَيَدْعُونَنَا رَغَبًا وَرَهَبًا ۖ وَكَانُوا لَنَا خَاشِعِينَ
“Hakika wao walikuwa wakikimbilia katika mambo ya kheri na wakituomba kwa matumaini na khofu na walikuwa Kwetu wenye kunyenyekea.”[1]
Kumukhofu kwao Allaah hakukuwafanya kukata tamaa na rehema za Allaah:
إِنَّهُ لَا يَيْأَسُ مِن رَّوْحِ اللَّـهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْكَافِرُونَ
“Hakika hawakati tamaa na faraja ya Allaah isipokuwa watu makafiri.”[2]
وَمَن يَقْنَطُ مِن رَّحْمَةِ رَبِّهِ إِلَّا الضَّالُّونَ
“Na nani anayekata tamaa na rehema za Mola wake isipokuwa waliopotea.”[3]
Sambamba na hilo kule kutaraji kwao kwa Allaah hakukufanya kuhisi wako salama kutokana na vitimbi vya Allaah. Allaah (Subhaanah) amesema:
أَفَأَمِنُوا مَكْرَ اللَّـهِ ۚ فَلَا يَأْمَنُ مَكْرَ اللَّـهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْخَاسِرُونَ
“Je, wameaminisha nja za Allaah? Basi hawaaminishi njama za Allaah isipokuwa watu wenye kukhasirika.”[4]
Baba wa Mitume Ibraahiym (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
وَاجْنُبْنِي وَبَنِيَّ أَن نَّعْبُدَ الْأَصْنَامَ
“… uniepushe mimi na wanangu kuabudu masanamu… “[5]
Ibraahiym (´alayhis-Salaam) hakujiaminisha nafsi yake, alichelea kupewa mtihani. Licha ya yote yeye ni mtu. Kwa ajili hiyo mtu asijiaminishe nafsi yake na akajiona kuwa ni mwema; bali anatakiwa kuchelea juu ya nafsi yake lakini pasi na kutaka tamaa na rehema za Allaah. Allaah (Ta´ala) amesema:
قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَى أَنْفُسِهِمْ لا تَقْنَطُوا مِنْ رَحْمَةِ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعاً إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ
“Sema: “Enyi waja Wangu ambao mmepindukia juu ya nasfi zenu: “Msikate tamaa na rehema za Allaah. Kwani hakika anasamehe madhambi yote. Kwani hakika Yeye ni mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[6]
Kwa hivyo ni lazima kwa mtu kufanya zile sababu zinazopelekea kupata rehema za Allaah, nazo ni kutubia na kujisalimisa kwa Allaah (Subhaanah). Hapo ndipo atapata rehema za Allaah. Rehema za Allaah ziko karibu kwa wafanyao mema. Wema ni sababu pia ya kupata rehema za Allaah.
[1]21:90
[2]12:87
[3]15:56
[4]7:99
[5]14:35
[6]39:53
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 261-262
- Imechapishwa: 21/05/2025

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 261-262
Imechapishwa: 21/05/2025
https://firqatunnajia.com/238-aqiydah-ya-kati-na-kati-baina-ya-usalama-na-kukata-tamaa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket