Katika ´Aqiydah Uislamu uko kati ya kufananisha na kukanusha. Bi maana kati ya kukanusha majina na sifa za Allaah, na kati ya kumfananisha kiumbe na Muumba. ´Aqiydah iko kati na kati. Mu´attwilah wanachupa mipaka katika kutakasa na hivyo wakakanusha majina na sifa za Allaah. Mushabbihah wamechupa mipaka katika kuthibitisha mpaka wakafikia kumfananisha Allaah na viumbe Wake. Hata hivyo ´Aqiydah ni kati na kati:
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖوَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.”[1]
Maneno Yake:
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye… “
wanaraddiwa Mushabbihah. Maneno Yake:
وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
“… Naye ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.”
wanaraddiwa Mu´attwilah. Sisi, Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, tunathibitisha yale majina na sifa ambazo Allaah amejithibitishia Mwenyewe na aliyomthibitishia nayo Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa msemo mwingine hatuzikanushi wala kuzipinga. Wala hatumfananishi Allaah na yeyote katika viumbe Wake. Bali tunaamini kuwa majina na sifa za Allaah zinalingana Naye (Subhaanah). Hata kama majina na sifa hizi zinapatikana kwa watu, lakini hata hivyo namna inatofautiana. Sifa ni yenye kumfuata yule mwenye kusifika nayo.
[1]42:11
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 259
- Imechapishwa: 21/05/2025
Katika ´Aqiydah Uislamu uko kati ya kufananisha na kukanusha. Bi maana kati ya kukanusha majina na sifa za Allaah, na kati ya kumfananisha kiumbe na Muumba. ´Aqiydah iko kati na kati. Mu´attwilah wanachupa mipaka katika kutakasa na hivyo wakakanusha majina na sifa za Allaah. Mushabbihah wamechupa mipaka katika kuthibitisha mpaka wakafikia kumfananisha Allaah na viumbe Wake. Hata hivyo ´Aqiydah ni kati na kati:
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖوَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.”[1]
Maneno Yake:
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye… “
wanaraddiwa Mushabbihah. Maneno Yake:
وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
“… Naye ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.”
wanaraddiwa Mu´attwilah. Sisi, Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, tunathibitisha yale majina na sifa ambazo Allaah amejithibitishia Mwenyewe na aliyomthibitishia nayo Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa msemo mwingine hatuzikanushi wala kuzipinga. Wala hatumfananishi Allaah na yeyote katika viumbe Wake. Bali tunaamini kuwa majina na sifa za Allaah zinalingana Naye (Subhaanah). Hata kama majina na sifa hizi zinapatikana kwa watu, lakini hata hivyo namna inatofautiana. Sifa ni yenye kumfuata yule mwenye kusifika nayo.
[1]42:11
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 259
Imechapishwa: 21/05/2025
https://firqatunnajia.com/236-aqiydah-ya-kati-na-kati-baina-ya-kufananisha-na-kukanusha/