23. Starehe na maisha – bila israfu wala majivuno

157 – Mahmuud bin Ghaylaan ametuhadithia: ´Abdus-Swamad bin ´Abdil-Waarith ametuhadithia: Hammaam ametuhadithia, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa ´Amr bin Shu´ayb, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba yake, ambaye amesimulia kwamba Mtume wa Allaah  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Kuleni, kunyweni, vaeni na toeni swadaqah bila israfu na bila majivuno. Hakika Allaah anapenda ionekane athari ya neema Zake kwa mja Wake.”[1]

158 – Muhammad bin Abaan ametuhadithia: Hakkaam ar-Raaziy ametuhadithia, kutoka kwa Sa´iyd bin Saabiq, kutoka kwa ´Aaswim, kutoka kwa Bakr bin ´Abdillaah al-Muzaniy, ambaye amesema:

”Vaeni nguo za wafalme na ziueni nyoyo zenu kwa khofu.”

159 – Muhammad bin ´Umar bin ´Aliy al-Muqaddamiy ametuhadithi: Kathiyr bin Hishaamametuhadithi: Nimemsikia Ja´far bin Burqaan akiulizwa na bwana mmoja:

”Unaonaje kuvaa sufu?” Akasema: ”Siipendi.” Akauliza: ”Na nguo za manyoya?” Akasema: ”Siipendi.” Akamuuliza: ”Basi ni ipi?” Akasema: ”Kama nguo zetu hizi, ukinunua mzigo wake – ukapata fadhilah kwa muuzaji, kisha ukaubeba hadi nyumbani kwako.” Mtu akasema: ”Hiyo si kama ilivyokuwa ile.”

160 – Muhammad bin Qudaamah ametuhadithia: Khaalid bin Khidaash ametuhadithia, kutoka kwa Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Hishaam, ambaye ameeleza:

”Aliambiwa Hind bint al-Muhallab: ”Kwa nini huachi kuvaa hariri?” Akasema: ”Sitaiacha mpaka iwe ndiyo kitendo changu kibaya zaidi.”

161 – Muhammad bin ´Abbaad al-Makkiy amenihadithia: Sufyaan ametuhadithia: Nimemsikia Ibn Shubrumah akisema:

”Hakika nguo ninayoichukia zaidi kwangu ni ile niliyowahi kuifanyia kazi.”

162 – Baba yangu amenihadithia: Ibraahiym bin Hiraasah ametuhadithia: Nimemsikia Sufyaan ath-Thawriy akisema:

”Nguo yenye manufaa zaidi kwako ni ile unayoidharau zaidi.”

[1] Ahmad (2/181). Cheni ya wappokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa Ahmad Shaakir.

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 198-204
  • Imechapishwa: 24/03/2026