Haya ndio mapokezi niliyoyapata kutoka kwa imamu huyu wa mji wa mahamio Maalik bin Anas (Rahimahu Allaah). Baadhi ya mapokezi ni Swahiyh na yamethibiti, na mengine yana kasoro. Hata hivyo yanatiana nguvu na kusapotiana. Hata hivyo mkusanyiko wa masimulizi yote hayo ni yenye kuthibiti pasi na shaka yoyote. Kwa ajili hiyo ndio maana wanazuoni wakayategemea. Kama tulivyotangulia kusema ni kwamba yamesahihishwa na wanazuoni wengi. Isitoshe haitambuliki kama kuna  yeyote ambaye ameyadhoofisha. Muda si mrefu tutanukuu maneno ya wanazuoni wakiyatapa na kuyasifu na kuyapokea kwa kuyakubali na kuyaonelea kuwa ni mazuri.

  • Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 41-42
  • Imechapishwa: 30/11/2025