Miongoni mwa madhara ya maasi ni kuwa yanaeneza juu ya ardhi ufisadi kama vile wa maji, hewa, mavuno, matunda na majengo. Amesema (Ta´ala):

ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِي النَّاسِ لِيُذِيقَهُم بَعْضَ الَّذِي عَمِلُوا لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ

“Ufisadi umedhihiri katika nchi kavu na baharini kwa sababu ya yale iliyochuma mikono ya watu ili [Allaah] awaonjeshe baadhi ya yale waliyotenda; huenda wapate kurejea.”[1]

Mujaahid amesema:

“Pindi dhalimu anaposhika utawala kunaenea dhuluma na ufisadi. Kwa ajili hiyo Allaah anaizuia mvua na matokeo yake mizizi na matunda vinaharibika – na Allaah hapendi ufisadi.” Kisha akasoma:

ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِي النَّاسِ لِيُذِيقَهُم بَعْضَ الَّذِي عَمِلُوا لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ

“Ufisadi umedhihiri katika nchi kavu na baharini kwa sababu ya yale iliyochuma mikono ya watu ili [Allaah] awaonjeshe baadhi ya yale waliyotenda; huenda wapate kurejea.”[2]

Kisha akasema:

“Ninaapa kwa Allaah kwamba si bahari zenu peke yake. Kila kijiji kilicho na maji ni bahari.”

´Ikrimah amesema:

“Sizungumzii bahari zenu hapa. Nazungumzia kila kijiji kilicho na maji ni bahari.”

Qataadah amesema:

“Nchi iliyo imara ni miji na bahari ni vijiji na nchi.”

Allaah ameyaita maji matamu kuwa ni “bahari” na akasema:

وَمَا يَسْتَوِي الْبَحْرَانِ هَـٰذَا عَذْبٌ فُرَاتٌ سَائِغٌ شَرَابُهُ وَهَـٰذَا مِلْحٌ أُجَاجٌ

“Bahari mbili hazilingani: haya [maji] ladha yake ni matamu, yenye kukata kiu, mazuri kwa kunywa, na mengine ni yenye chumvi kali.”[3]

[1] 30:41

[2] 30:41

[3] 35:12

  • Mhusika: Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Daa’ wad-Dawaa’, uk. 75
  • Imechapishwa: 09/01/2018