99 – Abu Sa´iyd al-Hasan bin Muhammad bin ´Abdillaah bin Hasnuuyah al-Aswbahaaniy ametukhabarisha: Ahmad bin Ja´far bin Ma´bad as-Simsaar ametuhadithia: Abu Bakr bin an-Nu´maan ametuhadithia: Zayd bin ´Awf ametuhadithia: Ja´far bin Sulaymaan ametuhadithia, kutoka kwa Maalik bin Diynaar, ambaye amesema:

”Mwanachuoni asiyetendea kazi elimu yake ni kama vile jiwe lainI: tone linapotua juu yake, linatiririka tu.”

100 – Abul-Husayn Muhammad bin ´Abdil-Waahid bin ´Aliy al-Bazzaar ametukhabarisha: Abul-Qaasim ´Umar bin Muhammad bin Sayf al-Kaatib ametusomea: Muhammad bin al-´Abbaas al-Yaziydiy ametusomea: Abul-Fadhwl ar-Rayaashiy ametusomea:

Asiye msomi ni ambaye anasimulia elimu bila kuifanyia kazi

ambapo anajizuilia na matamanio

mpaka ayafanyie kazi yale aliyofunza –

na hapo anakuwa si mwenye kusimangwa

Ni mara chache kuna faida katika kuonelea sawa

Ikiwa matendo ya mtu si ya sawa

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 62-63
  • Imechapishwa: 13/05/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy