23. Hadiyth ”Wakati Mtume wa Allaah alipokuwa akiwaswalisha Maswahabah wake… ”

Abu Daawuud (1/247) amesema: Muusa bin Ismaa´iyl ametuhadithia: Hammaad bin Zayd ametuhadithia, kutoka kwa Abu Na´aamah as-Sa´diy, kutoka kwa Abu Nadhwrah, kutoka kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy, ambaye ameeleza:

”Wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa akiwaswalisha Maswahabah wake alivua viatu vyake na kuviweka upande wa kushotoni mwake. Wakati Maswahabah walipoona hivyo, nao pia walivua viatu vyao. Baada ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumaliza swalah yake akawauliza: “Kipi kimekupelekeeni kuvua viatu vyenu?” Wakasema: “Tulikuona ukivua viatu vyako, basi nasi tukavua vyetu.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Jibriyl (´alayhis-Salaam) amenijia na kunieleza kwamba vina najisi na ndio maana nikavivua. Mmoja wenu anapofika msikitini, basi aangalie viatu vyake. Ikiwa ataona najisi katika viatu vyake, basi aifute na aswali akiwa navyo.”[1]

Ameipokea Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” (1/384), Ibn Hibbaan, uk. 107 katika “Mawaarid-udh-Dhwamaan”, Ahmad (3/20), al-Haakim (1/260), ambaye amesema kuwa ni “Swahiyh kwa mujibu wa sharti za Muslim” na adh-Dhahabiy akaafikiana naye, ´Abdur-Razzaaq (1/388), Ibn Abiy Shaybah (2/416), Abu Daawuud at-Twayaalisiy (1/84), ad-Daarimiy (1/32), at-Twahaawiy (1/511), al-Bayhaqiy (2/431) na Ibn Hazm katika “al-Muhallaa” (1/93).

[1] Abu Daawuud (650). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (650).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 24
  • Imechapishwa: 19/06/2025