23. Asiyemkufurisha kafiri au anaona kuwa madhehebu yake ni sahihi

Swali 23:  Nini maana ya maneno ya Shaykh Muhammad bin Abd-il-Wahhaab katika kichenguzi cha tatu cha Uislamu:

“Yeyote ambaye hamkufurishi mshirikina, akatilia shaka juu ya ukafiri wao au akaonelea kuwa madhehebu yao ni sahihi basi yeye ni kama wao.”?

Jibu: Maana ya hili ni kwamba yeyote ambaye ataitakidi kwamba washirikina wako katika haki au akachukua msimamo wa kusimama katika hilo, basi ni kafiri, kwa sababu hakukufuru twaaghuut. Tawhiyd ni lazima yatimie mambo mawili:

1 – Kukufuru twaaghuut.

2 – Kumwamini Allaah.

Hiyo ndio maana ya ”hapana mungu isipokuwa Allaah”. Maana yake ni kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah.

Jumla isemayo ”hapana mwabudiwa wa haki” ni kukufuru waungu wa batili. Jumla isemayo ”isipokuwa Allaah” ni kumwamini Allaah.

Kwa hivyo yule ambaye hawakufurishi washirikina, mayahudi, manaswara au waabudia mizimu, au akachukua msimamo wa kusimama katika kuwakufurisha, basi ni mwenye kumkufuru Allaah. Ni lazima awe na yakini na aone kuwa ni makafiri. Hivyo mwenye kusema:

“Mayahudi na manaswara wanayo dini ya mbinguni vivyo hivyo na waislamu wote wako katika haki.”

ni kafiri, kwa sababu hakuwakufurisha washirikina. Kwa hivyo ni lazima aitakidi kuwa mayahudi na manaswara wako katika batili na kwamba ni makafiri. Akitilia shaka au akachukua msimamo wa kunyamaza, basi jambo hilo linachengua Uislamu wake na anakuwa kafiri. Vivyo hivyo inahusiana na ambaye ataona kuwa madhehebu yao ni sahihi na akasema kuwa manaswara na mayahudi wako katika haki na kwamba ni sawa mtu akitaka kuamini dini ya uyahudi, ukristo au ya Uislamu, huyo ni kafiri kwa sababu ameona kuwa madhehebu yao ni sahihi.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 53-54
  • Imechapishwa: 08/01/2026