al-Qummiy amesema wakati alipofasiri Kauli ya Allaah:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَسْتَحْيِي أَن يَضْرِبَ مَثَلًا مَّا بَعُوضَةً فَمَا فَوْقَهَا

“Hakika Allaah Haoni hayaa kupiga mfano wa mbu na ulio zaidi yake.” (02:26)

“Baba yangu amenieleza, kutoka kwa an-Nadhr bin Suwayd, kutoka kwa Qaasim bin Sulaymaan, kutoka kwa al-Ma´aalaa bin Khunays, kutoka kwa Abu ´Abdillaah ambaye amesema: “Huu ni mfano Allaah Amepiga kwa kiongozi wa waumini (Rahimahu Allaah). Mbu ni kiongozi wa waumini na ulio zaidi yake ni Mtume wa Allaah. Dalili ya hilo ni Kauli Yake:

فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا فَيَعْلَمُونَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ

“Basi wale walioamini huelewa kwamba hiyo ni haki kutoka kwa Mola wao.”

Bi maana kiongozi wa waumini ambaye Mtume wa Allaah alichukua ahadi na waumini:

وَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا فَيَقُولُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّـهُ بِهَـٰذَا مَثَلًا ۘيُضِلُّ بِهِ كَثِيرًا وَيَهْدِي بِهِ كَثِيرًا

“Ama wale waliokufuru husema: “Anataka nini Allaah kwa mfano huu?” [Allaah] Huwapoteza kwa mfano huu wengi na Hawaongozi kwa mfano huu wengi na wala Hawapotezi kwayo ila mafasiki… “

Allaah Akawaraddi kwa kusema:

وَمَا يُضِلُّ بِهِ إِلَّا الْفَاسِقِينَ الَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ اللَّـهِ مِن بَعْدِ مِيثَاقِهِ

“… Hawapotezi kwayo ila mafasiki. Wale ambao wanavunja ahadi ya Allaah baada ya kuifunga Kwake.” (02:26-27)

Bi maana ahadi na ´Aliy:

وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّـهُ بِهِ أَن يُوصَلَ

“… na wanayakata Aliyoamrisha kwayo Allaah kuungwa… “

Bi maana kufunga bendi na kiongozi wa waumini (Rahimahu Allaah) na maimamu:

وَيُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ

“… na wanafanya ufisadi katika ardhi. Hao ndio wenye khasara.”[1]

Hakuna kitu kilicho kidogo na chenye kudharauliwa kama mbu. Kutafsiri ya kwamba mbu ni ´Aliy na kilicho zaidi yake kuwa ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni dharau na ukiukaji usiokuwa na mfano na upotoshaji wa Kitabu cha Allaah na malengo yake makubwa ya ubaya na dharau za Baatwiniyyah.

Moja katika malengo ya Baatwiniyyah na upotoshaji huu ni kutaka kuwakufurisha viumbe bora baada ya Mtume na watu wenye kushikamana na dini ya Allaah ya haki na Qur-aan tukufu kutokana na ´Aqiydah, ´ibaadah na Jihaad. Walihakikisha mambo makubwa ambayo hakuna yeyote baada ya Mitume waliyafanya wala watayafanya.

Aayah hizi mbili zinawasifu waumini kwa jumla na khaswa Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Pindi Allaah Anapopiga mfano katika Qur-aan wanauamini. Amewalaumu makafiri na wanafiki ambao wanaikadhibisha na kuipinga Qur-aan na mifano yake na wanavunja ahadi ya Allaah. Wanavunja ahadi zote na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), watu wengine hata wao kwa wao.

Ni ahadi ipi waliyovunja Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Enyi wanafiki! Ni amri ipi ambayo Allaah Ameamrisha kuifunga wakaivunja?

Kubadilisha ujumbe wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao ni manufaa kwa walimwengu wote duniani na Aakhirah na unawakinga na shari zote duniani na Aakhirah kwenda kwa ´Aliy ni unafiki wa wazi kabisa ambao malengo yake ni kubatilisha ujumbe wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kufanya uonekana kwa sura mbaya kabisa. Huu ni shabiki wa kipofu kwa ´Aliy na kizazi chake kwa njia ya kwamba Allaah Hakumtuma Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) isipokuwa ni kwa sababu ya kuhakikisha ushabiki huu wa kipofu usiokuwa na kifani.

Enyi wapotevu wapumbavu! Ni lini fungamano hili lilifungwa?[2] Ni lini fungamano la ukhaliyfah wa ´Aliy na kizazi chake lilivunjwa? Je, ilikuwa sehemu ya Makkah au al-Madiynah? Suurat-ul-Baqarah iliteremshwa al-Madiynah. Vipi uhusiano wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake uliweza kuwa kwa njia nzuri kabisa iwezekanayo ikiwa kama walikuwa makafiri wanafiki?

Ninaapa kwa Allaah ya kwamba hakuna yeyote aliyezua uongo kwa Qur-aan, Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Maswahabah zake na kizazi chake kama Raafidhwah Baatwiniyyah. Mayahudi, manaswara hata wanafiki hawajafanya hivo.

[1] Tafsiyr al-Qummiy (01/35).

[2] Waongo wanadai ya kwamba fungamano hili lilifungwa kabla ya watu kuumbwa na wakati mwingine wanasema kuwa lilifungwa siku ya Ghadiyr Kumm. Yote mawili ni katika uongo wa Baatwiniyyah.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 55-57
  • Imechapishwa: 19/03/2017