Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

45 – Agano ambalo Allaah amelichukua kutoka kwa Aadam na kizazi chake ni haki.

MAELEZO

Anaashiria baadhi ya Hadiyth zinazotamka wazi ya kwamba Allaah (Ta´ala) ametoa dhuriya kutoka mgongoni mwa Aadam (´alayhis-Salaam). Katika maelezo kumetajwa nne katika hizo. Nimezitaja katika kitabu changu ”Dhwilaal-ul-Jannah fiy Takhriyj-is-Sunnah”. Katika maelezo niliyoashiria nimebagua usahihi uliyotajwa wa kupangusa katika Hadiyth ya ´Umar. Ilikuwa ni usahaulifu wangu na namuomba Allaah (Ta´ala) anisamehe kwa hilo. Nimezinduka na hivi sasa naona kuwa Hadiyth hiyo inatiliwa nguvu kupitia njia ambayo ni nzuri iliyosimuliwa na Abu Hurayrah, na pia imetajwa katika maelezo, na njia nyingine kupitia cheni ya wapokezi dhaifu iliyosimuliwa na Ibn ´Abbaas na ambayo vyanzo na kiwango chake kimatajwa katika maelezo yaliyotanguliwa kutajwa (203).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 38
  • Imechapishwa: 23/09/2024