Kuhani ni yule ambaye anadai kujua mambo yaliyofichikana. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametusimulia kuwa mashaytwaan husikiliza kwa kuibia, wakaiba neno ambapo baadaye wakawaeleza makuhani, ambapo na wao wakauchanganya na uwongo mia. Matokeo watu wakawasadikisha katika yale yote wanayoyasema kwa sababu ya neno moja alilosema. Allaah (Subhaanah) amesema:
هَلْ أُنَبِّئُكُمْ عَلَىٰ مَن تَنَزَّلُ الشَّيَاطِينُ تَنَزَّلُ عَلَىٰ كُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٍ يُلْقُونَ السَّمْعَ وَأَكْثَرُهُمْ كَاذِبُونَ
“Je, nikujulisheni wanaowateremkia mashaytwaan? Wanateremka juu ya kila mzushi mwenye kutenda dhambi. Wanaotega sikio na wengi wao ni waongo.”[1]
Ukuhani kabla ya kuja Uislamu ilikuwa mwingi. Katika kila kabila alikuwepo kuhani, ambaye wanahukumiana kwake na wanamuuliza juu ya mambo yaliyofichikana. Ulipokuja Uislamu ukasambaratisha ukuhani na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akakataza kwenda kwa makuhani. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwenye kumwendea kuhani na kumuuliza kitu, basi hazitokubaliwa swalah zake kwa siku arobaini.”[2]
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tena:
“Mwenye kumwendea kuhani au mpiga ramli ambapo akamsadikisha aliyoyasema, basi ameyakufuru yale aliyoteremshiwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[3]
Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoulizwa kuhusu makuhani akasema “Wao si lolote”[4] na “Mtu asiwaendee”[5].
Kuhani ni ambaye anadai kujua mambo yaliyofichikana kwa sababu ya matangamano yake na shaytwaan.
[1] 26:221-223
[2] Muslim (2230).
[3] Ahmad (9532), al-Haakim (15) na al-Bayhaqî (16273). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ul-Jaamiy´” (5939).
[4] Muslim (2228).
[5] Muslim (537).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 250-251
- Imechapishwa: 06/05/2025
Kuhani ni yule ambaye anadai kujua mambo yaliyofichikana. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametusimulia kuwa mashaytwaan husikiliza kwa kuibia, wakaiba neno ambapo baadaye wakawaeleza makuhani, ambapo na wao wakauchanganya na uwongo mia. Matokeo watu wakawasadikisha katika yale yote wanayoyasema kwa sababu ya neno moja alilosema. Allaah (Subhaanah) amesema:
هَلْ أُنَبِّئُكُمْ عَلَىٰ مَن تَنَزَّلُ الشَّيَاطِينُ تَنَزَّلُ عَلَىٰ كُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٍ يُلْقُونَ السَّمْعَ وَأَكْثَرُهُمْ كَاذِبُونَ
“Je, nikujulisheni wanaowateremkia mashaytwaan? Wanateremka juu ya kila mzushi mwenye kutenda dhambi. Wanaotega sikio na wengi wao ni waongo.”[1]
Ukuhani kabla ya kuja Uislamu ilikuwa mwingi. Katika kila kabila alikuwepo kuhani, ambaye wanahukumiana kwake na wanamuuliza juu ya mambo yaliyofichikana. Ulipokuja Uislamu ukasambaratisha ukuhani na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akakataza kwenda kwa makuhani. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwenye kumwendea kuhani na kumuuliza kitu, basi hazitokubaliwa swalah zake kwa siku arobaini.”[2]
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tena:
“Mwenye kumwendea kuhani au mpiga ramli ambapo akamsadikisha aliyoyasema, basi ameyakufuru yale aliyoteremshiwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[3]
Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoulizwa kuhusu makuhani akasema “Wao si lolote”[4] na “Mtu asiwaendee”[5].
Kuhani ni ambaye anadai kujua mambo yaliyofichikana kwa sababu ya matangamano yake na shaytwaan.
[1] 26:221-223
[2] Muslim (2230).
[3] Ahmad (9532), al-Haakim (15) na al-Bayhaqî (16273). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ul-Jaamiy´” (5939).
[4] Muslim (2228).
[5] Muslim (537).
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 250-251
Imechapishwa: 06/05/2025
https://firqatunnajia.com/229-makuhani/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket