Tunaamini kujitokeza kwa Mnyama ardhini kutoka maeneo pake. Allaah (Subhaanah) amesema:

وَإِذَا وَقَعَ الْقَوْلُ عَلَيْهِمْ أَخْرَجْنَا لَهُمْ دَابَّةً مِّنَ الْأَرْضِ تُكَلِّمُهُمْ أَنَّ النَّاسَ كَانُوا بِآيَاتِنَا لَا يُوقِنُونَ

“Na itakapowaangukia kauli [kwa uwazi wake] Tutawatolea mnyama atembeaye katika ardhi atakayewasemezesha [aseme] kwamba watu walikuwa hawana yakini na alama Zetu.”[1]

Mnyama huyu atamuweka alama muumini na kafiri, alama itayojulisha nani ni nani. Watazungumzishwa pia; baadhi watazungumzishwa kama waislamu, wengine watazungumzishwa kama makafiri. Hiyo ndio ya maneno Yake Allaah:

تُكَلِّمُهُمْ

“… atakayewasemezesha… “

Kwa maneno yasiyokuwa ya kawaida. Hakujathibiti chochote kuhusu maeneo atakapotokea, lakini hata hivyo tunaamini kujitokeza kwake katika maeneo anayoyajua Allaah. Amesema (Subhaanah):

وَإِذَا وَقَعَ الْقَوْلُ عَلَيْهِمْ أَخْرَجْنَا لَهُمْ دَابَّةً مِّنَ الْأَرْضِ تُكَلِّمُهُمْ أَنَّ النَّاسَ كَانُوا بِآيَاتِنَا لَا يُوقِنُونَ

“Na itakapowaangukia kauli [kwa uwazi wake] Tutawatolea mnyama atembeaye katika ardhi atakayewasemezesha [aseme] kwamba watu walikuwa hawana yakini na alama Zetu.”

[1] 27:82

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 248
  • Imechapishwa: 30/04/2025