Tunaamini kushuka kwa ´Iysaa mwana wa Maryam (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutoka mbinguni. Anaitwa al-Masiyh (المسيح) kwa sababu alikuwa akiwagusa (مسح) wagonjwa ambapo Allaah akawaponya. Anaitwa pia al-Masiyh wa uongofu. Kushuka kwake kutoka mbinguni kuja duniani katika zama za mwisho ni jambo limepokelewa kwa mapokezi mengi. Yule mwenye kupinga jambo hilo ni kafiri. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَإِنَّهُ لَعِلْمٌ لِّلسَّاعَةِ فَلَا تَمْتَرُنَّ بِهَا
“Na hakika yeye [kurudi kwake duniani] ni alama ya [kukurubia kwa] Qiyaamah; basi msiitilie shaka.”[1]
Katika kisomo kingine imekuja (لَعَلَم الساعة), bi maana alama ya kukaribia kwa Qiyaamah. Allaah (Subhaanah) amesema:
وَإِن مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ إِلَّا لَيُؤْمِنَنَّ بِهِ قَبْلَ مَوْتِهِ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكُونُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا
“Hakuna yeyote katika Ahl-ul-Kitaab isipokuwa atamwamini kabla ya kufa kwake na siku ya Qiyaamah atakuwa shahidi juu yao.”[2]
Haya yatatokea katika zama za mwisho. Kwa sababu al-Masiyh bado akingali hai huko mbinguni. Atakufa baada ya kutekeleza kazi kubwa aliyopewa. Hapo ndipo atakufa na kuzikwa kwenye ardhi, baada ya kumuua ad-Dajjaal, nguruwe, kuondosha kodi na kuhukumu kwa Uislamu.
[1] 43:61
[2] 4:159
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 247
- Imechapishwa: 30/04/2025
Tunaamini kushuka kwa ´Iysaa mwana wa Maryam (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutoka mbinguni. Anaitwa al-Masiyh (المسيح) kwa sababu alikuwa akiwagusa (مسح) wagonjwa ambapo Allaah akawaponya. Anaitwa pia al-Masiyh wa uongofu. Kushuka kwake kutoka mbinguni kuja duniani katika zama za mwisho ni jambo limepokelewa kwa mapokezi mengi. Yule mwenye kupinga jambo hilo ni kafiri. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَإِنَّهُ لَعِلْمٌ لِّلسَّاعَةِ فَلَا تَمْتَرُنَّ بِهَا
“Na hakika yeye [kurudi kwake duniani] ni alama ya [kukurubia kwa] Qiyaamah; basi msiitilie shaka.”[1]
Katika kisomo kingine imekuja (لَعَلَم الساعة), bi maana alama ya kukaribia kwa Qiyaamah. Allaah (Subhaanah) amesema:
وَإِن مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ إِلَّا لَيُؤْمِنَنَّ بِهِ قَبْلَ مَوْتِهِ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكُونُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا
“Hakuna yeyote katika Ahl-ul-Kitaab isipokuwa atamwamini kabla ya kufa kwake na siku ya Qiyaamah atakuwa shahidi juu yao.”[2]
Haya yatatokea katika zama za mwisho. Kwa sababu al-Masiyh bado akingali hai huko mbinguni. Atakufa baada ya kutekeleza kazi kubwa aliyopewa. Hapo ndipo atakufa na kuzikwa kwenye ardhi, baada ya kumuua ad-Dajjaal, nguruwe, kuondosha kodi na kuhukumu kwa Uislamu.
[1] 43:61
[2] 4:159
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 247
Imechapishwa: 30/04/2025
https://firqatunnajia.com/224-tunamuamini-kushuka-kwa-al-masiyh-kutoka-mbinguni/