Hakuna Mtume yeyote isipokuwa aliwatadharisha ummah wake kutokana na ad-Dajjaal, lakini Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemtahadharisha zaidi. Kwa sababu yeye ndiye Mtume wa mwisho na ummah wake ndio wa mwisho na ndio uko karibu zaidi na ad-Dajjaal. Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wakati mmoja wenu anapomaliza Tashahhud [ya mwisho] basi amuombe Allaah ulinzi kutokamana na mambo mane; adhabu ya Moto, adhabu ya kaburi, mtihani wa uhai na wa kifo na mtihani wa al-Masiyh ad-Dajjaal.”[1]

Kwa hivyo ni matihani na shari kubwa. Baadaye atashuka ´Iysaa (´alayhis-Salaam) kutoka mbinguni na kumuua karibu na mlango wa Ludd. Allaah awapumzishe waislamu kutokana naye. Baada ya hapo ´Iysaa ahukumu kwa hukumu ya Uislamu. Kwa maana nyingine atamfata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa sababu hakuna Nabii mwingine baada ya Mtume, wala hakuna Shari´ah nyingine baada ya Shari´ah ya Uislamu.

Katika wakati wa ´Iysaa atajitokeza Ya´juuj na Ma´juuj. Huo pia ni mtihani mwingine mkubwa. Allaah (Ta´ala):

حَتَّىٰ إِذَا فُتِحَتْ يَأْجُوجُ وَمَأْجُوجُ وَهُم مِّن كُلِّ حَدَبٍ يَنسِلُونَ

“… mpaka watakapofunguliwa Ya´juuj na Ma´juuj nao kutoka kila mwinuko watateremka.”[2]

Ni aina ya wana Aadam waliokuwa wakiishi wakati wa Aleksander wakati wa Dhul-Qarnayn. Yeye ndiye ambaye aliwajengea ukuta dhidi yao:

فَمَا اسْطَاعُوا أَن يَظْهَرُوهُ وَمَا اسْتَطَاعُوا لَهُ نَقْبًا

“Basi hawakuweza kuukwea, na wala hawakuweza kuutoboa.”[3]

Ukuta, ambao ni wa chuma, hawawezi kupanda juu yake na wala hawawezi kuuvunja kutokana na nguvu yake kubwa. Lakini wakati itapokuja ahadi ya Allaah, basi atakifanya kuvunjika ambapo watatoka na kueneza uharibifu katika ulimwengu. Hapo hakuna yeyote atakayeweza kuwapiga vita, kisha baadaye Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) atawaangamiza kwa mkupo mmoja.

[1] at-Tirmidhiy (3613) ambaye amesema Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.

[2] 21:96

[3] 18:97

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 246-247
  • Imechapishwa: 29/04/2025