Wapinzani wengi hawayajali haya kabisa. Pengine wengi hawajui hata elimu waliokuwa nayo maimamu hawa waliotajwa, sembuse kujua maneno na maafikiano ya Maswahabah na wanafunzi wao katika suala hili. Huenda mtu akamjia Allaah kumuomba msamaha ambapo wakampendekeza kujifunza misingi ya dini na kumtambua Allaah kwa dalili. Matokeo yake wakawatii na kushikilia mizunguko ya kielimu ambapo akatahadharishwa kutokana na ufanano na kuwa na kiwiliwili (التجسيم). Wakamshawishi kuwa Hanaabilah ni watu wenye kumfanya Allaah kuwa na kiwiliwili na wakamshtua eti wanasema kuwa Allaah yuko na mkono, kwamba yuko juu ya mbingu na mfano wa hayo…[1] Kumpenda Abu Bakr na ´Umar…[2] Sifa… Hatafakari hata yale yanayosemwa na wale wanaozithibitisha…[3] isipokuwa tu kuwa dhibi yao. Wala sio mwadilifu wakati anapohoji na wala si mwenye busara anapotafakari. Upande mmoja ni mwenye kupewa udhuru kwa kule kumkanushia Allaah kuwa na kiwiliwili, upande mwingine si mwenye kupewa udhuru kwa sababu hakutafakari kwa kina na kuelewa kwamba kuthibitisha sifa hakupelekei katika ufananishaji wala kumfanya Allaah kuwa na kiwiliwili. Kufananisha ni pale ambapo mtu atasema kuwa mkono wa Allaah ni kama mkono wetu. Lakini pindi mtu atasema kuwa mkono wa Allaah usiofanana na mikono mingine, kama ambavyo dhati Yake haifanani na dhati zingine, usikizi Wake haufanani na masikizi mengine, uoni Wake haufanani na maono mengine – hakuna tofauti kati ya yote hayo – huko ndio kutakasa.

[1] Utupu katika muswada.

[2] Utupu katika muswada.

[3] Utupu katika muswada.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy (afk. 748)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´iyn fiy Swifaati Rabb-il-´Aalamiyn, uk. 103-104
  • Imechapishwa: 05/06/2024