Ilikuwa ni wajibu kwako kutaja mafunzo ya Tawhiyd ambayo nimeyavunja ili kuwaonyesha watu yule mwenye kumkosoa Sayyid Qutwub amevunja mafunzo ya Tawhiyd. Ilikua ni wajibu vililevile kuonyesha yanayopelekewa na Tawhiyd ambayo nimevunja na yanayozungumzia maisha marefu ya Sayyid. Nataraji kabisa kuwa utabainisha jambo hili kubwa, nalo ni kuonyesha kwa mfano Tawhiyd katika maneno ya Sayyid Qutwub ili kuwazuia wale wenye kumkosoa na kuwalea Ummah juu ya mafunzo na misingi hii.

Kuhusu mimi, siyajui haya kwa Sayyid Qutwub. Sionelei kuwa yanazungumzia maisha yake marefu. Ninachojua kwake ni kwamba alikuwa ni mwanafunzi wa al-´Aqqaad, Twaahaa Husayn na mwanachama wa chama cha kisekula al-Wafd kwa muda wa miaka kumi na tano. Kwa miaka kumi na tano aliishi hali ya kuchanganyikiwa na mashaka. Alifikia hata kuwa na mashaka juu ya uwepo wa Allaah. Alikuwa na hamu ya kuingia kwa undani kusoma falsafa ya magharibi na utamaduni wa ulaya, marekani na tamaduni zingine. Haya yamesemwa na yeye mwenyewe na marafiki zake[1].

[1] Tazama Kitabu cha al-Khaalidiy ”Sayyid Qutwub – min al-Miylaad ilaa al-Istishhaad”, uk. 213-245.