Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaanini kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni mtu na hana sifa yoyote ile ya uungu na wala hajui mambo yaliyofichikana isipokuwa yale aliyofunuliwa na Allaah. Wakati mwingine (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaulizwa juu ya kitu katika hukumu za Shari´ah ambapo ananyamaza mpaka kwanza aletewe Wahy. Wakati mwingine anaweza kutoa neno na akajiwa na uvuaji au kutiwa sawa kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall). Siku moja aliulizwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kufa shahidi kunafanya mtu akasamehewa kila kitu ambapo akajibu: “Ndio.”

Kisha akasema: “Yuko wapi muulizaji?” Akasema: “Isipokuwa tu deni” amenijuza hayo Jibriyl hivi punde tu.”[1]

Wakati mwingine anajitahidi (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) lakini anajiwa na Wahy kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall) kwamba usawa ni namna hivi na vile ambavyo ni kinyume na vile alivyojitahidi (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Kwa hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni mja miongoni mwa waja wa Allaah na hana sifa yoyote ile ya uungu. Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah juu ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) matendo yake yamekatika kwa kufa kwake. Kama alivosema mwenyewe:

“Anapokufa mtu basi matendo yake hukatika isipokuwa mambo matatu; swadaqah yenye kuendelea, elimu ambayo watu wananufaika kwayo au mtoto mwema mwenye kumuombea.”[2]

Matendo aliyokuwa akifanya mwenyewe yamekatika. Lakini hapana shaka kwamba kila elimu tuliyojifunza kutoka kwenye Shari´ah ya Allaah ni kupitia yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hivyo anakuwa ni mwenye kunufaika na elimu zote hizi tulizojifunza baada ya kufa kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vivyo hivyo matendo mema tunayoyafanya yalikuwa kwa maelekezo yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hivyo anapata mfano wa ujira wa watendaji.

[1] Muslim (1885).

[2] al-Bukhaariy (2651) na Muslim (2535).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy-´Aqiydah wal-´Amal, uk. 34-35
  • Imechapishwa: 19/08/2019