Swali 22: Ni ipi dalili ya maneno ya muadhini katika swalah ya Fajr:
الصلاة خير من النوم
“Swalah ni bora kuliko usingizi.”?
Unasamaje kwa ambaye anasema:
حي على خير العمل
“Njooni katika tendo bora.”?
Je, neno hili lina msingi?
Jibu: Imethibiti kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha Bilaal na Abu Mahdhuurah kufanya hivo katika adhaana ya Fajr. Vilevile imethibiti kwamba Anas amesema:
“Miongoni mwa Sunnah ni muadhini kusema katika adhaana ya Fajr:
الصلاة خير من النوم
“Swalah ni bora kuliko usingizi.”
Ameipokea Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” yake.
Manen haya yanasemwa juu ya adhaana inayotolewa wakati kunapochomoza alfajiri kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni. Husemwa kuwa ni adhaana ya kwanza ukilinganisha na Iqaamah. Kwa sababu Iqaamah ndio adhaana ya pili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kuna swalah kati ya kila adhaana mbili.”
Vilevile imethibiti katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy kupitia kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) yanayojulisha hayo.
Kuhusu maneno ya baadhi ya Shiy´ah wanaosema:
حي على خير العمل
“Njooni katika tendo bora.”
ni Bid´ah na hayana msingi wowote katika Hadiyth Swahiyh. Tunamuomba Allaah awaongoze na waislamu wote katika kufata Sunnah na kuziuma kwa magego. Kwani, naapa kwa Allaah, ndio njia ya uokozi na ya furaha kwa Ummah mzima.
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 24-25
- Imechapishwa: 18/08/2022
Swali 22: Ni ipi dalili ya maneno ya muadhini katika swalah ya Fajr:
الصلاة خير من النوم
“Swalah ni bora kuliko usingizi.”?
Unasamaje kwa ambaye anasema:
حي على خير العمل
“Njooni katika tendo bora.”?
Je, neno hili lina msingi?
Jibu: Imethibiti kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha Bilaal na Abu Mahdhuurah kufanya hivo katika adhaana ya Fajr. Vilevile imethibiti kwamba Anas amesema:
“Miongoni mwa Sunnah ni muadhini kusema katika adhaana ya Fajr:
الصلاة خير من النوم
“Swalah ni bora kuliko usingizi.”
Ameipokea Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” yake.
Manen haya yanasemwa juu ya adhaana inayotolewa wakati kunapochomoza alfajiri kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni. Husemwa kuwa ni adhaana ya kwanza ukilinganisha na Iqaamah. Kwa sababu Iqaamah ndio adhaana ya pili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kuna swalah kati ya kila adhaana mbili.”
Vilevile imethibiti katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy kupitia kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) yanayojulisha hayo.
Kuhusu maneno ya baadhi ya Shiy´ah wanaosema:
حي على خير العمل
“Njooni katika tendo bora.”
ni Bid´ah na hayana msingi wowote katika Hadiyth Swahiyh. Tunamuomba Allaah awaongoze na waislamu wote katika kufata Sunnah na kuziuma kwa magego. Kwani, naapa kwa Allaah, ndio njia ya uokozi na ya furaha kwa Ummah mzima.
Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 24-25
Imechapishwa: 18/08/2022
https://firqatunnajia.com/22-kusema-%d8%a7%d9%84%d8%b5%d9%84%d8%a7%d8%a9-%d8%ae%d9%8a%d8%b1-%d9%85%d9%86-%d8%a7%d9%84%d9%86%d9%88%d9%85-fajr-kuna-dalili/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)