22. Hadiyth “Hakika katika bora ya masiku yenu ni siku ya ijumaa… ”

22 – ´Aliy bin ´Abdillaah ametuhadithia: Husayn bin ´Aliy al-Ju´fiy ametuhadithia: ´Abdur-Rahmaan bin Yaziyd bin Jaabir ametuhadithia, kutoka kwa Abul-Ash´ath as-Swan´aaniy, kutoka kwa Aws bin Aws, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

 (إن من أفضل أيامكم يوم الجمعة فيه خلق آدم، وفيه قبض، وفيه النفخة، وفيه الصعقة، فأكثروا عليَّ من الصلاة فإن صلاتكم معروضة عليَّ) . قالوا: يا رسول الله كيف تعرض عليك صلاتنا وقد أرمت؟ – يقولون: قد بليت – قال

(إن الله حرَّم على الأرض أن تأكل أجساد الأنبياء)

“Hakika katika bora ya masiku yenu ni siku ya ijumaa. Ndio siku ambayo ameumbwa Aadam na akafariki. Ndio siku ya Baragumu na ndio siku Kuzimia. Hivyo basi, kithiritisheni kuniswalia. Kwani hakika du´aa zenu naonyeshwa nazo. Wakasema: ”Ni vipi unaonyehswa du´aa zetu, ilihali umekwishateketea?” Akasema: ”Hakika Allaah ameuharamishia udongo kula miili ya Mitume.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh. Wanamme wake ni wanamme Swahiyh. Imetiwa kasoro kwa mambo yasiyotakikana. Ameipokea Abu Daawuud, Ibn Maajah, Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” na al-Haakim, ambaye ameisahihisha. Ahmad pia ameisahihisha. Kuna Hadiyth nyingine yenye kuitia nguvu kutoka kwa Abud-Dardaa’ na Abu Umaamah. Rejea katika “at-Targhiyb wat-Tarhiyb” (2/281), “al-Jalaa´’” (42-48), “Mishkaat-ul-Maswaabiyh” (1361) na “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (962).

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 37
  • Imechapishwa: 07/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy