219. Mtazamo wa kupindukia wa Suufiyyah juu ya mawalii

Maneno yake aliposema kuwa hamtumfadhilishi yeyote katika mawalii juu ya yeyote katika Manabii wanaraddiwa Suufiyyah, ambao wanachupa mipaka kwa mawalii. Wanaona kuwa ni wabora kuliko Mitume. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah hawapetuki mipaka kwa mawalii na kuwashusha nafasi zao wanazostahiki. Suufiyyah wapotofu wanawafadhilisha na kusema:

Nafasi ya Nabii iko katika nafasi iliyo

chini kidogo ya Mtume lakini ni chini ya walii[1]

Hii ni kufuru, kwa sababu Mitume ndio wabora. Kisha wanafuatia Manabii. Baada ya hapo ndio wanakuja mawalii. Kutokana na madai ya Suufiyyah kuwatanguliza kwao mawalii kabla ya Mitume, ni kwa sababu mawalii wanapokea moja kwa moja kutoka kwa Allaah lakinini Mitume wanapokea kupitia mjumbe.

Maneno yake mtunzi (Rahimahu Allaah):

“Tunasema kuwa Nabii mmoja ni bora kuliko mawalii wote.”

Haya hayana shaka yoyote. Mawalii wote, kuanzia kiumbe wa kwanza mpaka wa mwisho wao, hawalingani na Nabii mmoja tu. Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

[1]Tazama ”al-Futuuhaat al-Makkiyyah” (2/252) ya Ibn ´Arabiy.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 239-240
  • Imechapishwa: 28/04/2025