Maswahabah wanashindana ubora.Wabora wao ni wale makhaliyfah wanne: Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan na ´Aliy – Allaah awawie radhi wote. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema juu yao:
“Yule katika nyinyi atakayeishi kitambo kirefu basi ataona tofauti nyingi. Hivyo basi, lazimianeni na Sunnah zangu na Sunnah za makhaliyfah wangu waongofu na wenye kuognoza baada yangu. Ziumeni kwa magego. Nakutahadharisheni na mambo yaliyozuliwa, kwani hakika kila kitachozuliwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotofu.”[1]
Kisha wanafuatia wale wengine waliosalia ambao wamebashiriwa Pepo: Abu´Ubaydah ´Aamir bin al-Jarraah, Sa´d bin Abiy Waqqaas, Sa´iyd bin Zayd, az-Zubayr bin al-´Awaam, Twalhah bin ´Ubaydillaah na ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf – Allaah awawie radhi wote!
Halafu wanafuatia wale waliopigana vita vya Badr, kisha wale waliokula kiapo chini ya mti. Allaah (Ta´ala) amesema:
لَّقَدْ رَضِيَ اللَّـهُ عَنِ الْمُؤْمِنِينَ إِذْ يُبَايِعُونَكَ تَحْتَ الشَّجَرَةِ فَعَلِمَ مَا فِي قُلُوبِهِمْ فَأَنزَلَ السَّكِينَةَ عَلَيْهِمْ وَأَثَابَهُمْ فَتْحًا قَرِيبًا
”Hakika Allaah amewawia radhi waumini waliokupa kiapo cha usikivu na utiifu chini ya mti [Allaah] alijua yale yaliyomo nyoyoni mwao, basi akawateremshia utulivu na akawalipa ushindi wa karibu.”[2]
Kisha wanafuatia wale walioamini na wakapambana jihaad kabla ya Ushindi. Wao ni bora kuliko wale Maswahabah walioamini na wakapambana jihaad baada ya Ushindi. Allaah (Ta´ala) amesema:
لَا يَسْتَوِي مِنكُم مَّنْ أَنفَقَ مِن قَبْلِ الْفَتْحِ وَقَاتَلَ ۚ أُولَـٰئِكَ أَعْظَمُ دَرَجَةً مِّنَ الَّذِينَ أَنفَقُوا مِن بَعْدُ وَقَاتَلُوا ۚ وَكُلًّا وَعَدَ اللَّـهُ الْحُسْنَىٰۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ
“Hawi sawa miongoni mwenu aliyetoa kabla ya Ushindi na akapigana. Hao watapata daraja kuu kabisa kuliko wale waliotoa baada [ya ushindi] na wakapigana – na wote Allaah amewaahidi Pepo. Na Allaah kwa yote myatendayo ni Mwenye khabari.”[3]
Ushindi kunakusudiwa mkataba wa amani wa Hudaybiyyah.
Baada ya hapo wanafuatia Wahamiaji waliosalia na Wanusuraji waliosalia, kwa sababu Allaah (Ta´ala) ameanza kuwataja Wahamiaji kabla ya Wanusuraji pale aliposema:
وَالسَّابِقُونَالْأَوَّلُونَمِنَالْمُهَاجِرِينَوَالْأَنصَارِوَالَّذِينَاتَّبَعُوهُمبِإِحْسَانٍرَّضِيَاللَّـهُعَنْهُمْوَرَضُواعَنْهُ
“Wale waliotangulia mwanzoni ambao ni Muhaajiruun na Answaar na wale waliowafuata kwa wema, Allaah ameridhika nao nao wameridhika Naye.”[4]
Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu Wahamiaji:
لِلْفُقَرَاءِ الْمُهَاجِرِينَ الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَأَمْوَالِهِمْ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا وَيَنصُرُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ
“Wapatiwe pia mafuqara Muhaajiruun ambao wametolewa kutoka majumbani mwao na mali zao wanatafuta fadhilah na radhi kutoka kwa Allaah na wanamnusuru Allaah na Mtume Wake – hao ndio wakweli.”[5]
Kisha akasema (Subhaanah) kuhusu Wanusuraji:
وَالَّذِينَ تَبَوَّءُوا الدَّارَ وَالْإِيمَانَ مِن قَبْلِهِمْ يُحِبُّونَ مَنْ هَاجَرَ إِلَيْهِمْ وَلَا يَجِدُونَ فِي صُدُورِهِمْ حَاجَةً مِّمَّا أُوتُوا وَيُؤْثِرُونَ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ ۚ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ
“Na wale waliokuwa na makazi [Madiynah] na wakawa na imani kabla yao wanawapenda wale waliohajiri kwao na wala hawahisi choyo yoyote vifuani mwao kwa yale waliyopewa [Muhaajiruun] na wanawapendelea kuliko nafsi zao japokuwa wao wenyewe ni wahitaji. Na yeyote anayeepushwa na uchu wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu.”[6]
Amewatanguliza Wahamiaji na matendo yao kabla ya Wanusuraji na matendo yao, jambo ambalo linafahamisha kuwa Wahamiaji ndio bora zaidi. Kwa sababu wameiacha miji na mali zao kwa ajili ya kuhama kwa ajili ya Allaah. Hilo likajulisha ukweli wa imani yao.
[1]Abu Daawuud (4607), at-Tirmidhiy (2676) na Ibn Maajah (34). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniykatika ”al-Irwaa’” (2455).
[2]48:18
[3]57:10
[4]9:100
[5]59:8
[6]59:9
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 228-229
- Imechapishwa: 23/04/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)