Hili ni kama ni kama mfano wa Mu´tazilah, ambao ni miongoni mwa watu wenye mijadala na maneno mengi zaidi. Wameandika tafsiri za Qur-aan kwa misingi ya madhehebu yao. Baadhi ya tafsiri hizo ni kama ile ya ´Abdur-Rahmaan bin Kaysaan al-Aswamm, mwalimu wa Shaykh Ibraahiym bin Ismaa´iyl bin ‘Ulayyah ambaye alikuwa akijadiliana na Imaam ash-Shaafi’iy, Abu ´Aliy al-Jubba’iy, “at-Tafsiyr al-Kabiyr” ya hakimu ´Abdul-Jabbaar bin Ahmad al-Hamadhaniy, “al-Jaamiy´ li ´Ilm-il-Qur-aan” ya ´Aliy bin ´Iysaa ar-Rummaaniy na “al-Kashshaaf” ya Abul-Qaasim az-Zamakhshariy. Hawa na wengine kama wao walikuwa na I´tiqaad za Mu´tazilah.
Misingi mikuu ya Mu´tazilah ni mitano: Tawhiyd, uadilifu, daraja kati ya daraja mbili, kutekeleza matishio na kuamrisha mema na kukemea maovu. Tawhiyd yao ni ile ya Jahmiyyah ambayo ina maana ya kukanusha Sifa. Kutokana na msingi huo wanasema kuwa Allaah hatoonekana, kwamba Qur-aan ni kiumbe, kwamba Allaah (Ta´ala) hayuko juu ya viumbe na kwamba Hana ujuzi, uwezo, uhai, uoni, usikizi, maneno, matakwa wala sifa nyenginezo.
Kuhusu uadilifu wao wanamaanisha kwamba Allaah hakutaka kila kitu kinachotokea, hakuumba vyote na wala si muweza wa yote hayo. Kwa mtazamo wao wanaona kuwa si Allaah ndiye ameumba matendo ya waja, si yale mazuri wala yale mabaya. Hakuna Anachotaka, kwa mtazamo na wanavosema wao, isipokuwa yale aliyoamrisha Kishari´ah. Mengine yote hutokea pasi po matakwa Yake. ´Aqiydah hiyo wameenda sambamba nayo wale Shiy´ah waliokuja nyuma, kama vile al-Mufiyd na Abu Ja´far at-Twuusiy. Abu Ja´far anayo tafsiri ya Qur-aan kwa mujibu wa mfumo huu.
Miongoni mwa misingi yao, inayoenda sambamba na ya Khawaarij, ni kutekeleza matishio huko Aakhirah. Inahusiana na kwamba Allaah hatokubali maombezi kwa ajili ya wale watenda madhambi makubwa na kwamba hakuna yeyote katika wao atakayeondolewa Motoni. Hapana shaka yoyote kwamba sampuli mbilimbili ya makundi ya Murji-ah wamewaraddi, kama vile Karraamiyyah na Kullaabiyyah. Wakati fulani Radd zao ni nzuri na mara nyingine ni mbaya, na hivyo kujikuta wakiwa kinyume kabisa, kama ilivyoelezwa kwa kina mahali pengine.
Kilichokusudiwa ni kwamba watu kama hawa walikuwa na ´Aqiydah fulani waliyoamini kisha wakalazimisha matamshi ya Qur-aan yaendane na ´Aqiydah hiyo. ´Aqiydah yao haina rejeo lolote kutoka kwa Maswahabah, wale waliowafuata kwa wema wala maimamu wa waislamu, si katika maono yao wala katika tafsiri zao za Qur-aan.
- Muhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Muqaddimah fiy Usuwl-it-Tafsiyr, uk. 73-76
- Imechapishwa: 03/04/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket