Imaam Abu ´Abdillaah Ibn Battwah al-´Ukbariy amesema katika ”al-Ibaanah”:

“Mlango unaozungumzia ya kwamba Allaah yuko juu ya ´Arshi Yake hali ya kutengana na viumbe Vyake na kwamba ujuzi Wake umewazunguka viumbe Vyake wote. Waislamu wote, kutoka kwa Maswahabah na wanafunzi wao, wameafikiana ya kwamba Allaah yuko juu ya ´Arshi Yake, juu ya mbingu Zake, na hali ya kutengana na viumbe Vyake. Ama kuhusu maneno Yake:

هُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۚ يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِي الْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ السَّمَاءِ وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا ۖ وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ

“Yeye Ndiye aliyeumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ‘Arshi. Anajua yale yanayoingia ardhini na yale yatokayo humo na yale yanayoteremka kutoka mbinguni na yale yanayopanda humo – Naye yupamoja nanyi popote mlipo.”[1]

wanazuoni wanasema kwamba kunakusudiwa utambuzi Wake.”[2]

Imaam Abu ´Abdillaah Muhammad bin Ishaaq bin Mandah amesema katika ”Kitaab-us-Swifaat”:

”Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ni Mwenye kusifiwa na si kwamba hatambuliki, yupo na si Mwenye kuzungukwa. Ni Mwenye kuonekana, kana kwamba unamuona, bila ya kumzunguka kutokana na ukaribu Wake. Yuko wa karibu bila ya mgusano, Aliye mbali bila ya kukatika. Anasikia na anaona na amelingana juu ya ´Arshi. Moyo humtambua, lakini akili haiwezi kuelezea namna Yake na Yeye ni Mwenye kukizunguka kila kitu.”

Qaadhwiy na Imaam Abu Bakr Muhammad bin Twayyib al-Baaqillaaniy amesema:

”Mtu akiuliza kwamba Allaah si anasema kuwa yuko katika kila sehemu, tunamwomba hifadhi Allaah. Bali Yeye amelingana juu ya ´Arshi Yake, kama Alivyosema Mwenyewe (´Azza wa Jall):

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[3]

إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ

“Kwake linapanda neno zuri na tendo zuri hulitukuza.”[4]

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ أَمْ أَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ

“Je, mnadhani mko katika amani na aliyeko juu mbinguni kwamba hatokudidimizeni ardhini, tahamaki hiyo inatikisika? Au mnadhani mko katika amani na aliyeko juu mbinguni kwamba hatokutumieni tufani ya mawe basi mtajua vipi maonyo Yangu.”[5]

Akarefusha maneno katika suala hilo.

al-Bayhaqiy ameeleza ya kwamba Ibn Fawrak amesema kwamba ”amelingana juu” maana yake ni kwamba Amekuwa juu  na akasema kuhusiana na maneno Yake  (Ta´ala):

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ

“Je, mnadhani mko katika amani na aliyeko juu mbinguni kwamba hatokudidimizeni ardhini… ”

”Kwa maana Aliye juu ya mbingu.”

Imaam Abu Muhammad bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy al-Maghribiy amesema:

”Naye yujuu kabisa, Aliyetukuka, Mjuzi wa yote, Mwenye khabari ya kila kitu ambaye anakiendesha kila kitu, Muweza, Mwenye kusikia, Mwenye kuona, Aliye juu, Aliye mkubwa. Yeye yuko juu ya ´Arshi Yake kwa utukufu na kwa dhati Yake na yuko kila mahali kwa ujuzi Wake. Amemuumba mtu na anajua kile nafsi yake inamnong´oneza; na Yeye yuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake. Hakuna jani linalodondoka chini isipokuwa analijua wala punje katika giza la ardhi wala kinyevu na kikavu isipokuwa kimo katika kitabu kinachobainisha. Amemuumba mtu na anajua kile nafsi yake inamnong´oneza; na Yeye yuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake. Hakuna jani linalodondoka chini isipokuwa analijua wala punje katika giza la ardhi wala kinyevu na kikavu isipokuwa kimo katika kitabu kinachobainisha. Amelingana juu ya ´Arshi na ufalme Wake umezunguka.”[6]

Tayari tumeshatangulia kuleta maneno mfano wa haya kutoka kwa Muhammad bin ´Uthmaan bin Abiy Shaybah.

[1] 57:4

[2] al-Ibaanah (3/143).

[3] 20:5

[4] 35:10

[5] 67:16-17

[6] ar-Risaalah, uk. 35-37.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (afk. 744)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Kalaam ´alaa Mas-alat-il-Istiwaa’ ´alaal-´Arsh, uk. 76-78
  • Imechapishwa: 29/12/2025