Mtu wa haki ukimwambia kuwa amekosea katika dalili na Sunnah, anakubali kwa kuwa makusudio yake ni haki na makusudio yake sio kutafuta rai yake iweze kushinda. Ukimwambia “Ee fulani! Umekosea Sunnah, umekosea dalili”, anakubali na kujirudi.

Ama ukimwambia mtu anayefuata matamanio yake kwamba amekosea, basi anakasirika na kughadhibika. Hii ndio alama ya Ahl-ul-Ahwaa´ ya kwamba kila mmoja anataka matamanio yake ndio yashinde. Kuhusu mtu wa haki anachotaka ni haki iweze kushinda na yeye anatafuta haki. Haki ndio lengo la muumini, kila mahala anapokutana nayo anaichukua.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Sharh-is-Sunnah, uk. 56
  • Imechapishwa: 28/12/2017