Iswaam bin Yuusuf (Rahimahu Allaah) alipita karibu na Haatim al-Aswamm, ambaye alikuwa akizungumza kwenye kikao chake, ambapo akasema: “Ee, Haatim, hivi unajua kuswali?” Akasema: “Ndiyo.” Akasema: “Unaswalije?” Haatim akasema: “Nasimama kutokana na amri, natembea kwa khofu, naingia kwa nia, naleta Takbiyr kwa matukuzo, nasoma kwa utaratibu ipasavyo na kwa kuzingatia, narukuu kwa unyenyekevu, nasujudu kwa kujishusha, nakaa kwenye Tashahhud kikamilifu, naikamilisha kwa nia, natoa salamu kwa kumtakasia nia Allaah (‘Azza wa Jall) na hurejea kwa kuwa na khofu. Nakhofia nisije kutokukubaliwa. Isitoshe nailinda kwa bidii mpaka wakati wa kufa.” Akasema: “Zungumza, kwa sababu wewe unajua kuswali.”

  • Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Hanbaliy (afk. 795)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Khushuu´ fiys-Swalaah, uk. 82-83
  • Imechapishwa: 24/11/2025