9 – Upokezi wa Bashshar bin al-Khaffaaf ash-Shaybaaniy[1]
Ibn Maajah amesema: `Aliy bin Sa’iyd[2] ametuhadithia: Bashshaar bin al-Khaffaaf, au mtu mwingine, ametuhadithia:
“Nilikuwa kwa Maalik bin Anas alipojiliwa na bwana mmoja na kusema: “Ee Abû ´Abdillaah!
الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ
”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[3]
Amelingana juu vipi?”
Akaitaja iliyobaki, imekuja namna hii katika “Tahdhiyb-ul-Kamaal”[4].
Abul-Mudhwaffar as-Sam´aaniy amesema: Wamepokea kwamba Ja´far bin ´Abdillaah na Bishr[5] al-Khaffaaf wamesema:
“Tulikuwa kwa Maalik bin Anas alipojiliwa na mtu mmoja na kumuuliza kuhusu maneno Yake (Ta’ala) Yake:
الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ
”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[6]
Amelingana juu vipi?” Maalik akainamisha kichwa chake kwa muda mrefu na akaanza kutokwa na jasho. Kisha akasema: “Namna haifahamiki na Kulingana juu hakutambuliki[7]. Ni wajibu kuamini jambo hilo na kuulizia juu yake ni Bid´ah.” Mimi sikufikirii vyengine isipokuwa mpotevu.” Kisha akaamuru atolewe nje.”[8]
Hakuna shaka yoyote juu ya upokezi Bashshaar.
[1] Abu ´Uthmaan Bashshaar bin Muusaa al-Khaffaaf ash-Shaybaaniy. Amesimulia kutoka kwa Maalik na akasimuliwa na ´Aliy bin Sa’d an-Nasawiy amesimulia kutoka kwake. Amejeruhiwa na al-Bukhaariy, Yahyaa bin Ma’iyn, Abu Daawuud, an-Nasaa’iy, ´Aliy al-Madiyniy na wengineo. Ahmad bin Yahya bin al-Jaruudiy amesema:
“Nilimsikia Aliy – yaani al-Madiyniy – akimtaja Bashshaar bin Muusaa na kusema: “Hakuna mtu huko Baghdad ambaye alikuwa thabiti zaidi katika ´Aqiydah. Ni maoni mazuri yaliyoje ya Abu ´Abdillaah alikuwa nayo juu yake!”
Kwa maana ya Ahmad bin Hanbal. Tazama “Tahdhiyb-ul-Kamaal” (4/85-90).
[2] ´Aliy bin Sa´iyd an-Nasawiy kwa jina jengine an-Nasaa’iy. Ibn Hajar amesema juu yake:
“Alikuwa mkweli na mtu wa Hadiyth.” (Taqriyb-ut-Taqriyb)
[3] 20:05
[4] Tahdhiyb-ul-Kamaal (4/90) na (20/449).
[5] Pengine ni kosa la uandikaji.
[6] 20:05
[7] Imekuja namna hii katika marejeo yaliyonakiliwa. Hata hivyo sahihi ni ”Kulingana juu si kitu kisichotambulika”.
[8] Tafsiyr-ul-Qur-aan (3/320).
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 40-41
- Imechapishwa: 29/11/2025
9 – Upokezi wa Bashshar bin al-Khaffaaf ash-Shaybaaniy[1]
Ibn Maajah amesema: `Aliy bin Sa’iyd[2] ametuhadithia: Bashshaar bin al-Khaffaaf, au mtu mwingine, ametuhadithia:
“Nilikuwa kwa Maalik bin Anas alipojiliwa na bwana mmoja na kusema: “Ee Abû ´Abdillaah!
الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ
”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[3]
Amelingana juu vipi?”
Akaitaja iliyobaki, imekuja namna hii katika “Tahdhiyb-ul-Kamaal”[4].
Abul-Mudhwaffar as-Sam´aaniy amesema: Wamepokea kwamba Ja´far bin ´Abdillaah na Bishr[5] al-Khaffaaf wamesema:
“Tulikuwa kwa Maalik bin Anas alipojiliwa na mtu mmoja na kumuuliza kuhusu maneno Yake (Ta’ala) Yake:
الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ
”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[6]
Amelingana juu vipi?” Maalik akainamisha kichwa chake kwa muda mrefu na akaanza kutokwa na jasho. Kisha akasema: “Namna haifahamiki na Kulingana juu hakutambuliki[7]. Ni wajibu kuamini jambo hilo na kuulizia juu yake ni Bid´ah.” Mimi sikufikirii vyengine isipokuwa mpotevu.” Kisha akaamuru atolewe nje.”[8]
Hakuna shaka yoyote juu ya upokezi Bashshaar.
[1] Abu ´Uthmaan Bashshaar bin Muusaa al-Khaffaaf ash-Shaybaaniy. Amesimulia kutoka kwa Maalik na akasimuliwa na ´Aliy bin Sa’d an-Nasawiy amesimulia kutoka kwake. Amejeruhiwa na al-Bukhaariy, Yahyaa bin Ma’iyn, Abu Daawuud, an-Nasaa’iy, ´Aliy al-Madiyniy na wengineo. Ahmad bin Yahya bin al-Jaruudiy amesema:
“Nilimsikia Aliy – yaani al-Madiyniy – akimtaja Bashshaar bin Muusaa na kusema: “Hakuna mtu huko Baghdad ambaye alikuwa thabiti zaidi katika ´Aqiydah. Ni maoni mazuri yaliyoje ya Abu ´Abdillaah alikuwa nayo juu yake!”
Kwa maana ya Ahmad bin Hanbal. Tazama “Tahdhiyb-ul-Kamaal” (4/85-90).
[2] ´Aliy bin Sa´iyd an-Nasawiy kwa jina jengine an-Nasaa’iy. Ibn Hajar amesema juu yake:
“Alikuwa mkweli na mtu wa Hadiyth.” (Taqriyb-ut-Taqriyb)
[3] 20:05
[4] Tahdhiyb-ul-Kamaal (4/90) na (20/449).
[5] Pengine ni kosa la uandikaji.
[6] 20:05
[7] Imekuja namna hii katika marejeo yaliyonakiliwa. Hata hivyo sahihi ni ”Kulingana juu si kitu kisichotambulika”.
[8] Tafsiyr-ul-Qur-aan (3/320).
Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 40-41
Imechapishwa: 29/11/2025
https://firqatunnajia.com/21-masimulizi-ya-maalik-kwa-mujibu-wa-upokezi-wa-bashshaar-ash-shaybaaniy/