21. Hadiyth ”Wakati Mtume wa Allaah… ”

Ibn Abiy Shaybah (2/418) ametuhadithia: ´Affaan ametuhadithia: Hammaad bin Salamah ametuhadithia: Abu Na´aamah as-Sa´diy ametuhadithia, kutoka kwa Abu Nadhwrah, kutoka kwa Abu Sa´iyd, ambaye ameeleza:

”Wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaswali alivua viatu vyake na kuviweka upande wa kushotoni mwake.”

Hadiyth ni Swahiyh kwa mujibu wa sharti za Muslim.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 21
  • Imechapishwa: 04/06/2025