21. Alikuwa hatambuliki akiwa kati ya watumwa wake

143 – Yahyaa bin Yuusuf az-Zammiy ametuhadithia: Abul-Maliyh ametuhadithia, kutoka kwa Maymuun bin Mihraan, ambaye ameeleza:

”Ibn ´Umar alipofikiwa na mwanawe akamwambia: “Nivishe  kikoi.” Kikoi chake kilikuwa kimechakaa. Akamwambia: “Nenda ukikate kisha ukishone, hakika hiyo itakutosha. Naapa kwa Allaah! Ninakuona mtakuja kuweka mlichoruzukiwa na Allaah ndani ya matumbo yenu na juu ya ngozi zenu, na kuwaacha wajane wenu, mayatima wenu na masikini wenu.”

144 – ´Abdur-Rahmaan bin Waaqid amenihadithia: Dhamrah ametuhadithia, kutoka kwa Sa´d bin al-Hasan at-Tamiymiy, aliyesema:

”´Abdur-Rahmaan bin ´Awf hakuwa anajulikana kati ya watumwa wake.”

Kwa sababu ya unyenyekevu wake katika mavazi.

145 – Baba yangu amenihadithia: Yuunus bin Muhammad ametukhabarisha, kutoka kwa Ibn Abiy Laylaa, kutoka kwa Ibraahiym bin Abiy Hurrah, ambaye ameeleza ya kwamba ´Iysaa bin Maryam (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nguo nzuri ni kiburi cha moyo.”

146 – Abu Ja´far al-Aadamiy amenihadithia, kutoka kwa Muhammad bin Shariyk: Sa´iyd bin Saalim ametuhadithia, kutoka kwa al-Hasan bin Abiy Yaziyd al-´Ijliy, kutoka kwa Twaawuus, ambaye amesema:

“Ninapoosha nguo zangu hizi mbili, huwa najiona kama si mimi kwa sababu ya usafi wake.”

147 – Ibn Jamiyl ametuhadithia: ´Abdullaah bin al-Mubaarak ametuhadithia: ´Abdullaah bin Shawdhab ametukhabarisha: Nimemsikia Maalik bin Diynaar akisimulia kutoka kwa Abu Ghaalib, kutoka kwa Abud-Dardaa’, ambaye amesema:

Salman aliposafiri kwa miguu kutoka al-Madaa-in kwenda Shaam na alikuwa amevaa kisaa na suruali iliyokunjwa.”[1]

Ibn Shawdhab amesema:

“Salman alionekana akiwa amevaa vazi la kawaida lisilo na kofia na masikio yaliyoinama, ambayo ni mapana na marefu. Akaambiwa: “Umejifanya kuonekana vibaya.” Ndipo akasema: ”Hakika kheri ni kheri ya Aakhirah.”

148 – ´Abdur-Rahmaan bin Swaalih amenihadithia: Mansuur bin Abiy Nuwayrah amenihadithia, kutoka kwa al-Fudhwayl bin ´Iyaadhw, ambaye amesema:

”Salman alionekana amevaa joho la sufi, akaambiwa: “Kwani hujavaa laini kuliko hili?” Akasema: “Mimi ni mja, ninavaa kama mja. Nikikombolewa ndipo nitavaa mavazi yasiyochakaa pembezoni mwake.”

149 – Ishaaq bin Ibraahiym ametuhadithia: Ja´far bin Sulaymaan ametukhabarisha: Thaabit ametuhadithia, nadhani ni kutoka kwa Abu ´Uthmaan, ambaye amesema:

”Salman alipita karibu na madheheki wawili wa al-Madaa-in wakiwa weusi, walipomuona akiwa amefupisha nguo na mikono yake hadi nusu ya mkono, wakasema maneno ya dhihaka. Salmaan akadhani kuwa wanamtaja yeye, akamwambia mtu mmoja waliyekuwa naye: ”Wamesema nini?” Bwana yule akasema: ”Hakuna kitu.” Akasema: ”Nitakung´ang´ania mpaka unambie kile walichosema.” Akasema: ”Wamekufananisha na doli yenye furaha.” Ndipo Salmaan akasema: ”Hakika kheri ni kheri ya Aakhirah.”

[1] Nzuri.

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 184-189
  • Imechapishwa: 24/03/2026