Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio kizazi bora baada ya Mitume na Manabii. Hilo ni kwa sababu walikutana na Mteule (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wakamuamini, wakapambana geba kwa bega pamoja naye na wakasoma kutoka kwake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwapenda na Allaah akawachagua wawe ni Maswahabah wa Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah anasema:
لَّقَدْ رَضِيَ اللَّـهُ عَنِ الْمُؤْمِنِينَ إِذْ يُبَايِعُونَكَ تَحْتَ الشَّجَرَةِ فَعَلِمَ مَا فِي قُلُوبِهِمْ فَأَنزَلَ السَّكِينَةَ عَلَيْهِمْ وَأَثَابَهُمْ فَتْحًا قَرِيبًا
”Hakika Allaah amewawia radhi waumini waliokupa kiapo cha usikivu na utiifu chini ya mti [Allaah] alijua yale yaliyomo nyoyoni mwao, basi akawateremshia utulivu na akawalipa ushindi wa karibu.”[1]
مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّـهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ ۖ تَرَاهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا ۖ سِيمَاهُمْ فِي وُجُوهِهِم مِّنْ أَثَرِ السُّجُودِ ۚ ذَٰلِكَ مَثَلُهُمْ فِي التَّوْرَاةِ ۚ وَمَثَلُهُمْ فِي الْإِنجِيلِ كَزَرْعٍ أَخْرَجَ شَطْأَهُ فَآزَرَهُ فَاسْتَغْلَظَ فَاسْتَوَىٰ عَلَىٰ سُوقِهِ يُعْجِبُ الزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ ۗ وَعَدَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنْهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا
“Muhammad ni Mtume wa Allaah. Na wale walio pamoja naye ni wakali zaidi dhidi ya makafiri wanahurumiana baina yao. Utawaona wakirukuu na wakisujudu wakitafuta fadhilah na radhi kutoka kwa Allaah. Alama zao dhahiri zi katika nyuso zao kutokana na athari za sujudu. Huo ni mfano wao katika Tawraat na mfano wao katika Injiyl kama mmea umetoa chipukizi lake, likautia nguvu kisha likawa nene, kisha likasimama sawasawa juu ya shina lake liwapendezeshe wakulima ili kuwakasirisha makafiri. Allaah amewaahidi wale walioamini na wakatenda mema miongoni mwao msamaha na ujira mkubwa.”[2]
Maswahabah ndio watu wa karne bora. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Watu bora ni wa kizazi changu. Kisha wale watakaofuatia. Kisha wale watakaofuatia.”[3]
Kwa hivyo wao ndio karne bora kwa sababu ya usuhubiano wao na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuwapenda ni imani na kuwachukia ni unafiki. Allaah (Ta´ala) amesema:
لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ
”… ili kuwakasirisha makafiri.”
Kutokana na Aayah hii ni lazima kwa waislamu wote kuwapenda Maswahabah wote, kwa sababu Allaah (´Azza wa Jall) na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wanawapenda. Jengine ni kwa sababu walipambana jihaad katika njia ya Allaah, wakaeneza Uislamu Mashariki na Magharibi, wakamtukuza, wakamuamini, wakaifuata ile nuru aliyoteremshiwa. Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Allaah amesema kuhusu Wahamiaji na Wanusaraji:
لِلْفُقَرَاءِ الْمُهَاجِرِينَ الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَأَمْوَالِهِمْ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا وَيَنصُرُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ وَالَّذِينَ تَبَوَّءُوا الدَّارَ وَالْإِيمَانَ مِن قَبْلِهِمْ يُحِبُّونَ مَنْ هَاجَرَ إِلَيْهِمْ وَلَا يَجِدُونَ فِي صُدُورِهِمْ حَاجَةً مِّمَّا أُوتُوا وَيُؤْثِرُونَ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ ۚ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ
“Mafuqara Muhaajiruun ambao wametolewa kutoka majumbani mwao na [zikataifishwa] mali zao wanatafuta fadhila na radhi kutoka kwa Allaah na wanamnusuru Allaah na Mtume Wake – hao ndio wakweli. Na wale waliokuwa na makazi na wakawa na imani kabla yao wanawapenda wale waliohajiri kwao na wala hawapati kuhisi uzito wowote vifuani mwao kwa yale waliyopewa [Muhaajiruun] na wanawapendelea kuliko nafsi zao japokuwa wao wenyewe wako na njaa. Na yeyote anayeepushwa na ubakhili na tamaa ya uchu wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu. Na wale waliokuja baada yao wanasema: “Mola wetu! Tusamehe na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa imani na wala Usijaalie katika nyoyo zetu vifundo vya chuki kwa wale walioamini. Ee Mola wetu! Hakika Wewe ni Mwenye huruma, Mwenye kurehemu.”[4]
Hivo ndivo unakuwa msimamo wa waislamu kwa Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam); wanawaombea msamaha na wanamuomba asiweke vifundo ndani ya mioyo yao dhidi yao.
[1]48:18
[2]48:29
[3]al-Bukhaariy (2652) na Muslim (2533).
[4]59:8-10
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 226-227
- Imechapishwa: 22/04/2025

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 226-227
Imechapishwa: 22/04/2025
https://firqatunnajia.com/208-karne-ya-watu-bora/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket