Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah; wanamthibitishia Allaah (´Azza wa Jall) kughadhibika, kuridhia na sifa nyenginezo. Hata kama aina ya sifa hizi zipo kwa viumbe, lakini kuna tofauti:
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖوَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.”[1]
Viumbe pia wanasikia na kuona. Allaah amesema mwanzoni mwa Suurah hii:
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye… “
Ikafahamisha kuwa kuna tofauti kati ya sifa za Muumba na sifa za viumbe. Hiki ni kitu kinachotambulika ndani ya Qur-aan, Sunnah na ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.
Wapindishaji na wapotofu wanamkanushia Allaah majina na sifa Zake. Fikira yao ni eti sifa mfano wake zinapatikana kwa viumbe pia na endapo watazithibitisha itapelekea kumfananisha Allaah na viumbe. Ukweli wa mambo ni kuwa jambo hilo halipelekei kufananisha. Lakini fahamu hii ni tasa. Wanapindisha maana ya kughadhibika kwa Allaah kwamba ni kulipiza kisasi na kuridhia kwa Allaah ni kuneemesha. Badala yake ni wajibu kujisalimisha kwa Allaah na kwa Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na yale yaliyothibiti kutoka kwa wawili hao, na mtu aachane na batili na upindishaji huu. Kwa ajili hiyo alikuja kwa Imaam Maalik bin Anas na kumuuliza kuhusu maneno Yake:
الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ
“Mwingi wa rehema amelingana juu ya ‘Arshi.”[2]
na akauliza: “Amelingana juu vipi?” Akainamisha kichwa chake chini na kuanza kutokwa na jasho. Kisha akasema: “Kulingana kunatambulika. Namna haijulikani. Ni wajibu kuamini jambo hilo na ni uzushi kuuliza juu yake.”
[1]42:11
[2]20:5
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 224
- Imechapishwa: 21/04/2025
Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah; wanamthibitishia Allaah (´Azza wa Jall) kughadhibika, kuridhia na sifa nyenginezo. Hata kama aina ya sifa hizi zipo kwa viumbe, lakini kuna tofauti:
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖوَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.”[1]
Viumbe pia wanasikia na kuona. Allaah amesema mwanzoni mwa Suurah hii:
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye… “
Ikafahamisha kuwa kuna tofauti kati ya sifa za Muumba na sifa za viumbe. Hiki ni kitu kinachotambulika ndani ya Qur-aan, Sunnah na ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.
Wapindishaji na wapotofu wanamkanushia Allaah majina na sifa Zake. Fikira yao ni eti sifa mfano wake zinapatikana kwa viumbe pia na endapo watazithibitisha itapelekea kumfananisha Allaah na viumbe. Ukweli wa mambo ni kuwa jambo hilo halipelekei kufananisha. Lakini fahamu hii ni tasa. Wanapindisha maana ya kughadhibika kwa Allaah kwamba ni kulipiza kisasi na kuridhia kwa Allaah ni kuneemesha. Badala yake ni wajibu kujisalimisha kwa Allaah na kwa Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na yale yaliyothibiti kutoka kwa wawili hao, na mtu aachane na batili na upindishaji huu. Kwa ajili hiyo alikuja kwa Imaam Maalik bin Anas na kumuuliza kuhusu maneno Yake:
الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ
“Mwingi wa rehema amelingana juu ya ‘Arshi.”[2]
na akauliza: “Amelingana juu vipi?” Akainamisha kichwa chake chini na kuanza kutokwa na jasho. Kisha akasema: “Kulingana kunatambulika. Namna haijulikani. Ni wajibu kuamini jambo hilo na ni uzushi kuuliza juu yake.”
[1]42:11
[2]20:5
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 224
Imechapishwa: 21/04/2025
https://firqatunnajia.com/206-fahamu-tasa/