Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
152 – Anakimiliki kila kitu na hakuna kitu kinachommiliki. Hakuna yeyote anayejitosheleza na Allaah (Ta´ala) kwa kiasi cha kupepesa jicho. Ambaye anaona kuwa anaweza kujitosheleza na Allaah kiasi cha kupepesa jicho, basi amekufuru na amekuwa miongoni mwa waliokula khasara.
MAELEZO
Miongoni mwa sifa za Allaah (´Azza wa Jall) ni kwamba anamiliki kila kitu. Kila kilichoko ulimwenguni ni milki Yake:
تَبَارَكَ الَّذِي بِيَدِهِ الْمُلْكُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ
“Amebarikika Ambaye mkononi Mwake umo ufalme Naye juu ya kila jambo ni muweza.”[1]
لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ
“Ni Wake pekee ufalme wa mbingu na ardhi, anahuisha na anafisha, Naye juu ya kila jambo ni muweza.”[2]
Hakitoki chochote nje ya ufalme Wake. Watu na vile vyote wanavyomiliki ni milki Yake (Subhaanahu wa Ta´ala):
قُلِ اللَّـهُمَّ مَالِكَ الْمُلْكِ تُؤْتِي الْمُلْكَ مَن تَشَاءُ وَتَنزِعُ الْمُلْكَ مِمَّن تَشَاءُ وَتُعِزُّ مَن تَشَاءُ وَتُذِلُّ مَن تَشَاءُ ۖ بِيَدِكَ الْخَيْرُ ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ تُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَتُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ ۖ وَتُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَتُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ ۖ وَتَرْزُقُ مَن تَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ
“Sema: “Ee Allaah, mfalme uliyemiliki ufalme wote, unampa ufalme umtakaye, na unamwondoshea ufalme umtakaye, na unamtukuza umtakaye, na unamdhalilisha umtakaye, kheri imo mkononi mwako – hakika Wewe juu ya kila jambo ni muweza. Unauingiza usiku ndani ya mchana na unauingiza mchana ndani ya usiku na unatoa kilicho hai kutokana na kilicho mfu na unatoa kilicho mfu kutokana na kilicho hai na unamruzuku umtakaye bila ya hesabu.”[3]
Hakuna yeyote anaweza kumfaradhisha au kumlazimisha Allaah kitu. Kwa sababu watu ni waja wa Allaah na ni wenye kumuhitajia. Kama alivosema (Subhaanah):
وَرَبُّكَ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ وَيَخْتَارُ
“Mola wako anaumba na kuchagua Atakavyo.”[4]
إِنَّ اللَّـهَ يَفْعَلُ مَا يَشَاءُ
“Hakika Allaah anafanya atakavyo.”[5]
Yeye (Subhaanah) anayaendesha mambo na kuyafanya yapite kwa mujibu wa hekima Yake.
[1]67:1
[2]57:2
[3]3:26
[4]28:68
[5]22:18
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 222-223
- Imechapishwa: 20/04/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)