Kuna sampuli mbili za du´aa:

1 –Du´aa kwa njia ya ´ibaadah. Ni kule kumsifu Allaah (´Azza wa Jall) katika majina, sifa na matendo Yake. Yule mwenye kusema:

سبحان الله, الله أكبر, الحمد لله

“Allaah ametakasika kutokana na mapungufu, Allaah ni mkubwa na himdi zote njema anastahiki Allaah.”

Amemuomba du´aa ya ´ibaadah.

2 – Du´aa kwa njia ya kuomba. Nako ni pale mtu anapoomba mahitaji mbalimbali kwa Allaah (´Azza wa Jall). Zote mbili zimekusanywa na Suurah al-Faatihah. Mwanzoni mwake kuna du´aa kwa njia ya ´ibaadah, mpaka katika Aayah isemayo:

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

”Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada.”[1]

Mwishoni mwa Suurah kuna du´aa kwa njia ya maombi. Wanazuoni wanasema kuwa du´aa ya ´ibaadah inapelekea katika du´aa ya kuomba, ilihali du´aa ya kuomba inakusanya du´aa ya ´ibaadah.

[1]1:5

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 220
  • Imechapishwa: 16/04/2025