Swali 20: Nini maana ya maneno yao:

“Huu ni ukafiri kwa ajili ya kuonya.”?

Jibu: Maana yake ni kuwa huu ni ukafiri mdogo ambao haumtoi mtu katika Uislamu. Ni onyo linalokusudia kumzuia mtu kufanya tendo hilo. Hicho hicho kinaitwa ”ukafiri” ili akomeke na kitendo hicho. Haina maana kwamba ni ukafiri mkubwa.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah wa Ajwibah fiy-Iymaan wal-Kufr, uk. 50
  • Imechapishwa: 08/01/2026