Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) sade:

Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الرَّزَّاقُ ذُو الْقُوَّةِ الْمَتِينُ

”Hakika Allaah ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu kali madhubuti.” (51:58)

MAELEZO

Aayah zilizotaja utashi, matakwa na kadhalika. Zote hizi zinaonyesha ukubwa Wake (Subhaanah), kwamba Yeye ana utashi kamilifu, matakwa kamilifu, ujuzi kamili na uwezo kamilifu. Zote hizi ni sifa Zake (Jalla wa ´Alaa). Lakini hata hivyo zinatakiwa kuthibitishwa kwa njia isiyofanana na viumbe. Bi maana Anazo nguvu lakini sio kama nguvu za viumbe. Yeye nguvu Zake ni kamilifu kabisa. Vivyo hivyo inahusiana na sifa Zake zingine zote. Siza Zake zote ni kamilifu. Kwa ajili hii ndio maana amesema:

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye.” (42:11)

فَلَا تَضْرِبُوا لِلَّـهِ الْأَمْثَالَ

“Basi msimpigie mifano!” (16:74)

هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا

“Je, unamjua [mwengine] mwenye jina kama Lake?” (19:65)

وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ

“… na wala hana yeyote anayefanana [wala kulingana] Naye.” (112:04)

Ujuzi Wake ni kamilifu na sio kama ujuzi wa viumbe. Hakuna chochote chenye kujificha Kwake. Vivyo hivyo hekima Yake, uwezo Wake, nguvu Zake, upole Wake, usikizi Wake na uoni Wake. Zote hizi ni sifa kamilifu. Sifa hizi hazina upungufu wowote ndani yake. Hili ni tofauti na sifa za viumbe ambapo zina upungufu na ni dhaifu. Kuhusu Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) sifa Zake zote ni kamilifu. Amesema (Ta´ala):

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (42:11)

Hili ni kutokana na ukamilifu Wake:

هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا

“Je, unamjua [mwengine] mwenye jina kama Lake?” (19:65)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 28-29
  • Imechapishwa: 19/10/2024