20. Mwanamke haadhini wala hakimu

Swali 20: Je, kuadhini na kukimu ni jambo limesuniwa kwa mwanamke? Ni mamoja watakuwa katika hali ya ukazi peke yao au shambani mmojammoja au kwa mkusanyiko?

Jibu: Haikusuniwa kwa wanawake kuadhini wala kukimu. Ni mamoja watakuwa katika hali ya ukazi au ya safari. Hakika si venginevyo kuadhini na kukimu ni katika mambo maalum kwa wanamme. Hivo ndivo zimejulisha Hadiyth Swahiyh kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 23
  • Imechapishwa: 17/08/2022