2 – Msafiri ambaye mwezi wa Ramadhaan umemkuta akiwa safarini au ameanzisha safari katikati ya mwezi, safari yenye urefu usiopungua 80 km. Huo ndio umbali uliokuwa ukikatwa zamani kwa miguu au kwa mizigo katika muda wa siku mbili kwa mwendo wa kawaida. Msafiri huyu inapendekezwa kwake kufungua. Ni mamoja iwe swawm inamletea uzito au hapana kwa ajiliya kuchukua ruhusa. Ni mamoja iwe safari yake ni ya dharurah au ni endelevu, kama dereva wa teksi ambaye muda wake mwingi huwa safarini kati ya miji. Huyu hufungua katika safari yake na hufunga wakati wa ukaaji wake.
Msafiri akirejea katika nchi yake katikati ya mchana, basi inamlazimu kujizuia kula na kunywa sehemu iliyobaki ya mchana, kisha kuilipa siku hiyo kama ilivyotangulia.
Msafiri akinuia akiwa safarini kukaa zaidi ya siku nne, basi inamlazimu kufunga na kukamilisha swalah kama wakazi wengine, kwa sababu hukumu za safari humkatikia. Ni mamoja iwe ukaaji wake ni kwa masomo, biashara au jambo jingine. Ikiwa atanuia kukaa siku zisizozidi nne au akakaa kwa ajili ya kutimiza haja asiyojua itakamilika lini, basi anaruhusiwa kufungua kwa sababu bado yumo katika hukumu ya safari.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 26-27
- Imechapishwa: 11/02/2026
2 – Msafiri ambaye mwezi wa Ramadhaan umemkuta akiwa safarini au ameanzisha safari katikati ya mwezi, safari yenye urefu usiopungua 80 km. Huo ndio umbali uliokuwa ukikatwa zamani kwa miguu au kwa mizigo katika muda wa siku mbili kwa mwendo wa kawaida. Msafiri huyu inapendekezwa kwake kufungua. Ni mamoja iwe swawm inamletea uzito au hapana kwa ajiliya kuchukua ruhusa. Ni mamoja iwe safari yake ni ya dharurah au ni endelevu, kama dereva wa teksi ambaye muda wake mwingi huwa safarini kati ya miji. Huyu hufungua katika safari yake na hufunga wakati wa ukaaji wake.
Msafiri akirejea katika nchi yake katikati ya mchana, basi inamlazimu kujizuia kula na kunywa sehemu iliyobaki ya mchana, kisha kuilipa siku hiyo kama ilivyotangulia.
Msafiri akinuia akiwa safarini kukaa zaidi ya siku nne, basi inamlazimu kufunga na kukamilisha swalah kama wakazi wengine, kwa sababu hukumu za safari humkatikia. Ni mamoja iwe ukaaji wake ni kwa masomo, biashara au jambo jingine. Ikiwa atanuia kukaa siku zisizozidi nne au akakaa kwa ajili ya kutimiza haja asiyojua itakamilika lini, basi anaruhusiwa kufungua kwa sababu bado yumo katika hukumu ya safari.
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 26-27
Imechapishwa: 11/02/2026
https://firqatunnajia.com/20-msafiri-anaruhusiwa-kutofunga-ramadhaan/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket