4- Baadhi ya wale wenye kufuata kichwa mchunga wana dhana mbovu inayowazuia kutokamana na kufuata Sunnah inayoenda kinyume na madhehebu yao. Wanafikiria kwamba kule kufuata kwao Sunnah ni kuwatia makosani wale wale watu wenye madhehebu hayo. Kwa mujibu wao wanaona kuwa ni kumponda yule imamu. Ikiwa haifai kumtukana muislamu wa kawaida. Mtu aseme nini juu ya maimamu wao?
Uelewa huu ni batili na unatokana na kwamba hawaifahamu Sunnah. Vinginevyo ni vipi muislamu anaweza kusema kitu kama hicho? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye aliyesema:
“Atapohukumu hakimu na akajitahidi ambapo akapatia, basi ana ujira mmoja. Na atapohukumu na akajitahidi ambapo akakosea, basi ana ujira mara mbili.”[1]
Hadiyth hii inaraddi uelewa huo. Inabainisha vilevile kwamba mwenye kukosea anapata ujira mara moja. Ni vipi mtu atafikiria matusi kwa kitu kama hicho? Hapana shaka kwamba fikira hizi ni za batili na ni wajibu kwa kila mwenye kuonelea hivo ajirudi – vinginevyo yeye ndiye mwenye kuwatukana waislamu. Na si kwamba amemtukana muislamu mmoja mmoja katika wao, bali wale maimamu wao wakubwa katika Maswahabah, Taabi´uun na maimamu waliokuja baada yao. Kwani hakika sisi tunajua yakini kabisa kwamba watukufu hawa walikuwa wakitiana makosani wao kwa wao na baadhi wakiwaraddi wengine[2]. Hivi kweli mwenye akili timamu anaweza kusema kwamba baadhi walikuwa wakiwatukana wengine? Bali imesihi kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimtia makosani Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh) wakati alipofasiri ndoto iliokuwa imeonwa na mtu mmoja ambapo akasema:
“Umepatia baadhi ya mambo na umekosea baadhi ya mengine.”[3]
Hivi (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alizingatiwa amemtukana Abu Bakr kwa kusema hivo?
Kilicho cha ajabu zaidi kuliko hawa, ni kwamba wanaacha kufuata Sunnah inayoenda kinyume na madhehebu yao kwa sababu hapo wanaona kuwa watahesabika kwamba wamemtukana imamu wao. Sambamba na hilo wanaona kuwa ni kumuheshimu na kumuadhimisha iwapo watamfuata katiak kitu kinachoena kinyume na Sunnah. Kwa ajili hiyo wanaendelea kumfuata kiupofu. Hata hivyo wanasahau kuwa wanatumbukia kwenye kitu kibaya zaidi kuliko kile wanachojaribu kukikimbia. Ikiwa nyinyi mnamuheshimu imamu wenu pale mnapomfuata na ni kumtukana pale mnapoenda kinyume naye, ni vipi mmejijuzishia wenyewe kwenda kinyume na Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na badala yake kumfuata imamu wa madhehebu ambaye hakulindwa na kukosea na kumtukana sio jambo la kufuru? Ikiwa kule kumuasi imamu kwa mtazamo wenu mnaona kuwa ni kumtukana, basi kule kumuasi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kumtukana zaidi, bali ni jambo la ukafiri.
[1] al-Bukhaariy (6919) na Muslim (1716).
[2] Tazama maneno ya al-Imaam al-Muzaniy na Haafidhw Ibn Rajab yaliyotangulia punde.
[3] al-Bukhaariy na Muslim. Tazama ”al-Ahaadiyth as-Swahiyhah” (121).
- Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 63-64
- Imechapishwa: 23/01/2019

Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 63-64
Imechapishwa: 23/01/2019
https://firqatunnajia.com/20-haramu-kumuasi-imamu-lakini-si-mtume/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)