87 – Ishaaq bin Ibraahiym ametukhabarisha: Jariyr ametukhabarisha, kutoka kwa Huswayn, kutoka kwa Hilaal, kutoka kwa ´Abdullaah bin Dhwaalim, ambaye ameeleza:
“Niliingia kwa Sa’iyd bin Zayd na kusema: “Je, hushangazwi na dhalimu huyu anayewaamuru wahubiri kumtukana ´Aliy?” Akasema: ”Anafanya hivo? Nashuhudia kwamba watu tisa wamo Peponi, na lau ningeshuhudia watu kumi ningelisema kweli. Tulikuwa pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) pale Hiraa’ pale ilipoanza kutetemeka. Kisha akasema: “Tulia, Hiraa’! Hakuna aliye juu yako isipokuwa Nabii, mkweli au shahidi.” Nikasema: “Ni nani aliyekuwa juu ya Hiraa’?” Akasema: ”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), Abu Bakr, Umar, `Uthmaan, `Aliy, Twalhah, az-Zubayr, `Abdur-Rahmaan na Sa’d.” Tukasema: ”Ni nani aliyekuwa wa kumi?” Akasema: “Mimi.”[1]
88 – Ishaaq bin Ibraahiym ametukhabarisha: Ibn Idriys ametukhabarisha: Nimemsikia Huswayn akisimulia cheni ya wapokezi sawa na cheni hii.
Hilaal bin Yasaaf hakuisikia kutoka kwa ´Abdullaah bin Dhwaalim.
89 – Ishaaq bin Ibraahiym ametukhabarisha: ´Ubaydullaah bin Sa´iyd ametukhabarisha: Sufyaan ametukhabarisha: Mansuur ametukhabarisha, kutoka kwa Hilaal bin Yasaaf, kutoka kwa Ibn Hayyaan, kutoka kwa ´Abdullaah bin Dhwaalim, kutoka kwa Sa´iyd bin Zayd, ambaye amesema:
”Hiraa´ ilitikisika, ambapo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akasema… ”
90 – Muhammad bin al-Muthannaa ametukhabarisha: Yahyaa bin Sa´iyd ametukhabarisha: Swadaqah bin al-Muthannaa ametukhabarisha: Babu yangu Rabaah bin al-Haarith amenihadithia kutoka kwa Sa´iyd bin Zayd aliyesema:
”Siwezi kumzulia wa Allaah Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) uwongo, ambao atakuja kuniuliza nao pale nitapokutana naye, nashuhudia ya kwamba nimemsikia kwa masikio yangu na kuyaelewa na moyo wangu ya kuwa amesema: “Abu Bakr yuko Peponi, ´Umar yuko Peponi, ´Aliy yuko Peponi, ´Uthmaan yuko Peponi, Twalhah na az-Zubayr wako Peponi, ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf yuko Peponi na Sa´d bin Maalik yuko Peponi.” Ningelitaka kumtaja wa tisa basi ningelimtaja.” Watu waliokuweko msikitini wakaanza kumwomba na kusema: ”Ee Swahabah wa Mtume wa Allaah! Wewe ndiye wa tisa?” Akasema: ”Mmeniomba kwa jina la Allaah, Aliye Mtukufu. Mimi ndiye muumini wa tisa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ndiye wa kumi.”
[1] Abu Daawuud (4648) na at-Tirmidhiy (3757). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Ibn Maajah” (134).
- Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 75-76
- Imechapishwa: 09/09/2026

Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 75-76
Imechapishwa: 09/09/2026
https://firqatunnajia.com/20-fadhilah-za-saiyd-bin-zayd/