20. Dalili juu ya mkono wa Allaah 6

20- Abu Muhammad bin Sa´iyd ametuhadithia: Muhammad bin Zanbuur ametuhadithia: Fudhwayl bin ´Iyaadh ametuhadithia, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa ´Umar bin Salamah, kutoka kwa Abu ´Ubaydah, kutoka kwa Abu Muusa aliyeeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) humnyooshea mkono Wake aliyetenda dhambi usiku ili atubie mchana na aliyetenda dhambi mchana ili atubie usiku mpaka jua lichomoze kutoka magharibi.”

Ameipokea Muslim katika mlango unaohusu tawbah kupitia kwa Abu Muusa, kutoka kwa Ghundur, kutoka kwa Bundaar, kutoka kwa Abu Daawuud, kutoka kwa Shu´bah, kutoka kwa ´Amr.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 55-56
  • Imechapishwa: 05/11/2017