19. Dalili juu ya mkono wa Allaah 5

18- Abu Saalih al-Aswbahaaniy ´Abdur-Rahmaan bin Sa´d ametuhadithia: ´Aqiyl bin Yahyaa ametuhadithia: Sufyaan bin ´Uyaynah ametuhadithia: Abuz-Zinaad ametuhadithia, kutoka kwa al-A´raj, kutoka kwa Abu Hurayrah aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) amesema: “Ee mwanaadamu! Toa hivyo na mimi nitakupa. Hakika mkono wa kuume wa Allaah umejaa na unatoa daima. Hakuna kinachofanya ukapungua mchana na usiku.”

Ameipokea Muslim katika mlango unaohusu zakaah kupitia kwa az-Zuhayr, kutoka kwa Ibn Numayr, kutoka kwa Sufyaan bin ´Uyaynah.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 54-55
  • Imechapishwa: 05/11/2017