Maimamu wa waislamu, ambao ni Maswahabah na wale waliowafuata kwa wema, walikuwa wakishikamana na mfumo na njia moja katika suala hili. Hapakuwa kati yao makinzano wala tofauti. Bali wote, kuanzia wa mwanzo mpaka wa mwisho wao, kwa himdi za Allaah, walikuwa wakithibitisha yale yaliyothibitishwa na Qur-aan na Sunnah. Hawakuzipindisha maana, kuzipotosha. Hawakuweza kukanusha chochote katika hayo, kuzifananisha wala kuzirudisha nyuma. Hakuna yeyote katika wao ambaye aliona zinahitaji kufasiri chochote katika hizo kwa mafumbo. Bali walizipokea kwa kuzikubali na kujisalimisha na wakazikubali kwa kuziamini na kuzitukuza. Walichukua msimamo mmoja kwa zote na kuzifikisha kwa namna moja. Hawakufanya kama walivofanya watu wa matamanio na wazushi ambao wameifanya Qur-aan kuwa si yenye kutegemewa, wakakubali sehemu yake na kukataa sehemu yake nyingine bila ya dalili ya wazi[1].
Mu´attwilah walienda mbali zaidi. wakafanya kule kupinga na kumkanushia Mola sifa ni upwekeshaji, sambamba na hilo kule kumthibitishia nazo Allaah ni kumfananisha, kumfanya kuwa na kiwiliwili na kumfanya ni mwenye kupandiana. Wakaiita batili kuwa ni haki kwa ajili ya kuwakimbiza watu na kupambapamba kwa lengo la kuwavutia watu. Haki wakaiita batili kwa lengo la kuwashtua watu. Watu wengi huenda tu na mkumbo. Hawana uwezo wa wakosoaji wa kukosoa[2].
Hakuna awezaye kujikinga na upotofu katika jambo hili la khatari isipokuwa tu yule ambaye ana elimu ya Salaf na akapita njia yao. Njia yao ni salama na yenye amani ambayo inayo elimu na hekima. Maneno yao juu ya upwekeshaji na mengineyo ni machache lakini yenye baraka nyingi. Hawakuwa wenye kuyafanya mambo kuwa magumu. Bali walikuwa wakiyatukuza maandiko, wakitambua utukufu wake na wakikomeka nayo. Hawakuwa wakiyavuka kwa maoni, akili, kuonelea kitu kizuri au kitu kingine chochote. Walikuwa, kwa haki kabisa, ni maimamu watukufu na mashahidi imara. Sifa zote njema ni stahiki ya Allaah ambaye anafanya katika kila zama kuwepo wanazuoni katika kipindi cha kukatika Mitume. Wanazuoni hao wanaowaita wale waliopotea kwenda katika uongofu na wanawavumilia maudhi yao. Wanahuisha kwa Kitabu cha Allaah wale wafu, na wanawafanya kuweza kuona kwa nuru ya Allaah wale vipofu. Ni wangapi waliouliwa na Ibliys wamewahuisha! Ni wapotofu wangapi waliodanga ambao wamewaongoza! Ni athari nzuri iliyoje walionao kwa watu na ni ubaya uliyoje athari ya watu dhidi yao! Wanakilinda Kitabu cha Allaah upotoshaji wa waliochupa mipaka, madai ya watu wa batili na upindishaji wa maana wa wajinga; watu ambao wamechochewa kwa bendera za Bid´ah na kufungua njia za fitina. Wametofautiana juu ya Kitabu, wanaenda kinyume na Kitabu na wamekusanyika juu ya kufarikiana na Kitabu. Wanasema juu ya Allaah na juu ya Kitabu cha Allaah pasi na elimu. Wanazungumza maneno yasiyokuwa wazi na wanawahadaa wajinga katika watu katika wanayowababaisha. Tunamuomba Allaah ulinzi kutokana na fitina zinazopotosha[3].
[1] Tazama “Madaaridj-us-Saalikiyn” (1/49) ya Ibn-ul-Qayyim.
[2] Tazama “Madaaridj-us-Saalikiyn” (1/26-27) ya Ibn-ul-Qayyim.
[3] Tazama “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah”, uk. 55-57 ya Imaam Ahmad.
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 6-7
- Imechapishwa: 26/11/2025

Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 6-7
Imechapishwa: 26/11/2025
https://firqatunnajia.com/2-njia-moja-pekee-ndio-inayolinda-dhidi-ya-aqiydah-mbovu/