Haafidhw Ibn Hajar al-´Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

01- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Maji yake ni masafi na maiti yake ni halali.”[1]

Wameipokea watano na Ibn Abiy Shaybah na tamko ni lake. Imesahihishwa na Ibn Khuzaymah, at-Tirmidhiy, Maalik, ash-Shaafi´iy na Ahmad.

MAELEZO

Kusema kwamba maji yake ni masafi ni jambo lenye kuenea na linahusu maji yote ya bahari, maji ya mabwawa na maji ya mvua. Yote ni masafi. Kanuni ya hilo ni kwamba maji yote ambayo yanateremka kutoka mbinguni na chemchem inayotoka ardhini ni masafi na ni yenye kusafisha. Maji yenye kutiririka ni masafi ni mamoja yaanyoka kwenye mabonda yanayopita, mito au vinamasi. Yote hayo ni masafi, ni mamoja yamepitikiwa na muda mrefu au mfupi.

Unapofika katika kinamasi basi wewe tawadha kutoka hapo na oga. Usianze kuuliza kama ni najisi au twahara. Msingi ni kwamba ni masafi.

[1] Abu Daawuud (83), at-Tirmidhiy (69), an-Nasaa’iy (59), Ibn Maajah (386), Ibn Abiy Shaybah (1/131), Ibn Khuzaymah (111), Maalik (43), ash-Shaafi´iy katika ”al-Musnad” (1/7) na Ahmad (14594).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mukhtaswar ´alaa Buluugh-il-Maraam (1/22-23)
  • Imechapishwa: 26/04/2020