´Aliy al-Halabiy ni katika watu wabaya zaidi wanaoshuhudia batili. Anashuhudia kwa watu wapotevu na wenye misingi ilioharibika na mifumo batili ya kwamba ni Salafiyyuuun, amesimama upande wao na kutumia misingi na mifumo yao. Miongoni mwa watu hawa ni:
1- ´Adnaan ´Ar´uur
Mtu huyu ameeneza fitina na kuwapiga vita Ahl-us-Sunnah kwa miaka mingi. Ameeneza fitina kwa miaka mingi kwa kuwatetea wapotevu na khaswa Sayyid Qutwub ambaye amezungumza kwa Wahdat-ul-Wujuud, kukanusha Sifa za Allaah (´Azza wa Jall), kumfanyia mzaha na kumtukana Mtume wa Allaah Muusa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kuwatukana Maswahabah wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa matusi makali kama kusema ya kwamba [´Uthmaan bin ´Affaan] alivunja roho na msingi wa Kiislamu, kuukejeli ukhaliyfah wake na kuoenela kuwa ilikuwa ni pengo kati ya ukhaliyfah wa Abu Bakr na ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) na ukhalifah wa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu) na matusi mengine mengi. Rejea katika kitabu changu “Matwaa´in Sayyid Qutwub fiy Aswhaab Rasuulillaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)”.
Sayyid Qutwub amemtukana Mu´aawiyah na ´Amr bin al-´Aasw (Radhiya Allaahu ´anhumaa) na kuwatuhumu uongo, ghushi, khiyaana, unafiki na rushwa. Amewatuhumu waarabu wengi kuritadi ili baadaye kurudi kumtukana Mu´aawiyah (Radhiya Allaahu ´anhu). Rejea katika kitabu cha Sayyid Qutwub “Kutub wa Shakhswiyyaat[1]“.
´Adnaan anamtetea Sayyid Qutwub na kumpiga vita mwenye kumkosoa kwa haki. Anamsifu na anafanya hivo kwa uongo pindi anaposema kuwa hakuna yeyote aliyeasisi misingi kama alivofanya yeye. Huku anawatuhumu Salafiyyuun kuwa wanakosa misingi. Anamlinganisha na Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah, Ibn-ul-Qayyim na Ibn ´Abdil-Wahhaab wakati anapobainisha Tawhiyd na aina zake.
´Ar´uur amebuni misingi mingi ya batili ikiwa ni pamoja na:
“Tunasahihisha na wala hatujeruhi.”
“Ukihukumu na wewe utahukumiwa.”
Amebuni misingi sita ili kuweza kupiga vita mfumo wa Salaf kwayo na khaswa Jar wa Ta´diyl, kujeruhi na kusifu, ili kuwatetea wapotevu na kuwapiga vita Salafiyyuun.
Wanachuoni walifikiwa na khabari ya misingi hii, fitina, khatari na upotevu ambapo wakamnasihi ili aweze kuiacha, lakini akakataa. Kwa hivyo wakabainisha mfumo na msingi wake batili ambapo akawa amewatukana, akawafanyia mzaha na kuwakejeli. Wakati ´Allaamah Ibn ´Uthaymiyn alipoulizwa kuhusu kanuni zake akairaddi na kubainisha batili yake. Pamoja na hivyo mtu huyu akaendelea katika njia hiyo hiyo mpaka hii leo.
Ameandika kitabu kinachoitwa “Mahaj-ud-Da´wah fiy Dhwaw´-il-Waaqi´ al-Mu´aaswir” ambapo amejenga juu yake misingi yake potevu. Humo ameharamisha kwa wale wanaolingania katika Dini ya Allaah kuwahukumu wapotevu na akaenda mbali zaidi kiasi cha kwamba akaonelea kuwa ni haramu kwa Manabii kuwahukumu maadui wa Allaah makafiri. Anatumia hoja juu ya hilo kwa Aayah kama:
وَإِنَّمَا أَنَا نَذِيرٌ مُّبِينٌ |
||
“Na hakika mimi ni mwonyaji tu bayana.” (67:26) | ||
|
||
وَمَا أَنتَ عَلَيْهِم بِوَكِيلٍ |
||
“Na wewe hukuwakilishwa juu yao.” (06:107) |
Wakati huo huo akaendelea kushikamana na hukumu za Mitume kwa nyumati zao kwa kufuru, uongo na mengineyo.
Anazifumbia macho hukumu za Salaf juu ya wapotevu, waongo na wengineo ambao wamejaza vitabu kwa Jarh na Ta´diyl kwa jumla na khaswa vitabu vya Jarh na Ta´diyl. Hakutosheka na upotevu huu mpaka alipowaita watu wote ikiwa ni moja na mayahudi na manaswara katika umoja wa dini na kuzingatia kushikamana kwa mayahudi na manaswara na Tawrat iliyopotoshwa na Injiyl iliyopotoshwa ni kushikamana na kamba ya Allaah.
Aliwakilisha mkataba wa taifa la watu wa Syria – mkataba uliojengwa juu ya uanasekula, uhuru na mfumo wa wapotevu na haukujengwa juu ya ´Aqiydah ya Uislamu wala Shari´ah.
Pamoja na upotevu wote huu ambao unaenda kinyume na misingi na matawi ya Kiislamu unamuona jinsi al-Halabiy amesimama upande wake na kusema kuwa ni Salafiy. Amefanya hivo hata baada ya yeye kuita katika umoja wa dini, kuwasifu baadhi ya Nusayriyyah na kuwafadhilisha na kuwapa kipaumbele mbele ya waislamu na kuunda mkataba wa kisekula.
Je, ushuhudiaji wa al-Halabiy juu ya Salafiyyah ya ´Ar´uur hauzingatiwi kuwa ni katika ushuhudiaji wa batili ilio kubwa na wa aina mbaya zaidi? Je, ushuhudiaji huu hauendani kinyume na mfumo wa Salaf bali Uislamu?
[1] uk. 242-243.
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://rabee.net/ar/articles.php?cat=8&id=236
- Imechapishwa: 08/01/2017
´Aliy al-Halabiy ni katika watu wabaya zaidi wanaoshuhudia batili. Anashuhudia kwa watu wapotevu na wenye misingi ilioharibika na mifumo batili ya kwamba ni Salafiyyuuun, amesimama upande wao na kutumia misingi na mifumo yao. Miongoni mwa watu hawa ni:
1- ´Adnaan ´Ar´uur
Mtu huyu ameeneza fitina na kuwapiga vita Ahl-us-Sunnah kwa miaka mingi. Ameeneza fitina kwa miaka mingi kwa kuwatetea wapotevu na khaswa Sayyid Qutwub ambaye amezungumza kwa Wahdat-ul-Wujuud, kukanusha Sifa za Allaah (´Azza wa Jall), kumfanyia mzaha na kumtukana Mtume wa Allaah Muusa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kuwatukana Maswahabah wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa matusi makali kama kusema ya kwamba [´Uthmaan bin ´Affaan] alivunja roho na msingi wa Kiislamu, kuukejeli ukhaliyfah wake na kuoenela kuwa ilikuwa ni pengo kati ya ukhaliyfah wa Abu Bakr na ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) na ukhalifah wa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu) na matusi mengine mengi. Rejea katika kitabu changu “Matwaa´in Sayyid Qutwub fiy Aswhaab Rasuulillaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)”.
Sayyid Qutwub amemtukana Mu´aawiyah na ´Amr bin al-´Aasw (Radhiya Allaahu ´anhumaa) na kuwatuhumu uongo, ghushi, khiyaana, unafiki na rushwa. Amewatuhumu waarabu wengi kuritadi ili baadaye kurudi kumtukana Mu´aawiyah (Radhiya Allaahu ´anhu). Rejea katika kitabu cha Sayyid Qutwub “Kutub wa Shakhswiyyaat[1]”.
´Adnaan anamtetea Sayyid Qutwub na kumpiga vita mwenye kumkosoa kwa haki. Anamsifu na anafanya hivo kwa uongo pindi anaposema kuwa hakuna yeyote aliyeasisi misingi kama alivofanya yeye. Huku anawatuhumu Salafiyyuun kuwa wanakosa misingi. Anamlinganisha na Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah, Ibn-ul-Qayyim na Ibn ´Abdil-Wahhaab wakati anapobainisha Tawhiyd na aina zake.
´Ar´uur amebuni misingi mingi ya batili ikiwa ni pamoja na:
“Tunasahihisha na wala hatujeruhi.”
“Ukihukumu na wewe utahukumiwa.”
Amebuni misingi sita ili kuweza kupiga vita mfumo wa Salaf kwayo na khaswa Jar wa Ta´diyl, kujeruhi na kusifu, ili kuwatetea wapotevu na kuwapiga vita Salafiyyuun.
Wanachuoni walifikiwa na khabari ya misingi hii, fitina, khatari na upotevu ambapo wakamnasihi ili aweze kuiacha, lakini akakataa. Kwa hivyo wakabainisha mfumo na msingi wake batili ambapo akawa amewatukana, akawafanyia mzaha na kuwakejeli. Wakati ´Allaamah Ibn ´Uthaymiyn alipoulizwa kuhusu kanuni zake akairaddi na kubainisha batili yake. Pamoja na hivyo mtu huyu akaendelea katika njia hiyo hiyo mpaka hii leo.
Ameandika kitabu kinachoitwa “Mahaj-ud-Da´wah fiy Dhwaw´-il-Waaqi´ al-Mu´aaswir” ambapo amejenga juu yake misingi yake potevu. Humo ameharamisha kwa wale wanaolingania katika Dini ya Allaah kuwahukumu wapotevu na akaenda mbali zaidi kiasi cha kwamba akaonelea kuwa ni haramu kwa Manabii kuwahukumu maadui wa Allaah makafiri. Anatumia hoja juu ya hilo kwa Aayah kama:
وَإِنَّمَا أَنَا نَذِيرٌ مُّبِينٌ
“Na hakika mimi ni mwonyaji tu bayana.” (67:26)
إِنَّمَا أَنتَ مُنذِرٌ
“Hakika wewe ni mwonyaji tu.” (13:07)
وَمَا أَنتَ عَلَيْهِم بِوَكِيلٍ
“Na wewe hukuwakilishwa juu yao.” (06:107)
Wakati huo huo akaendelea kushikamana na hukumu za Mitume kwa nyumati zao kwa kufuru, uongo na mengineyo.
Anazifumbia macho hukumu za Salaf juu ya wapotevu, waongo na wengineo ambao wamejaza vitabu kwa Jarh na Ta´diyl kwa jumla na khaswa vitabu vya Jarh na Ta´diyl. Hakutosheka na upotevu huu mpaka alipowaita watu wote ikiwa ni moja na mayahudi na manaswara katika umoja wa dini na kuzingatia kushikamana kwa mayahudi na manaswara na Tawrat iliyopotoshwa na Injiyl iliyopotoshwa ni kushikamana na kamba ya Allaah.
Aliwakilisha mkataba wa taifa la watu wa Syria – mkataba uliojengwa juu ya uanasekula, uhuru na mfumo wa wapotevu na haukujengwa juu ya ´Aqiydah ya Uislamu wala Shari´ah.
Pamoja na upotevu wote huu ambao unaenda kinyume na misingi na matawi ya Kiislamu unamuona jinsi al-Halabiy amesimama upande wake na kusema kuwa ni Salafiy. Amefanya hivo hata baada ya yeye kuita katika umoja wa dini, kuwasifu baadhi ya Nusayriyyah na kuwafadhilisha na kuwapa kipaumbele mbele ya waislamu na kuunda mkataba wa kisekula.
Je, ushuhudiaji wa al-Halabiy juu ya Salafiyyah ya ´Ar´uur hauzingatiwi kuwa ni katika ushuhudiaji wa batili ilio kubwa na wa aina mbaya zaidi? Je, ushuhudiaji huu hauendani kinyume na mfumo wa Salaf bali Uislamu?
[1] uk. 242-243.
Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: http://rabee.net/ar/articles.php?cat=8&id=236
Imechapishwa: 08/01/2017
https://firqatunnajia.com/2-al-halabiy-na-aruur/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)