Kuhusu matendo mengine kuna makinzano. Allaah (Subhaanah) amesema:
وَأَن لَّيْسَ لِلْإِنسَانِ إِلَّا مَا سَعَىٰ
“… na mtu hatopata [malipo] isipokuwa yale aliyoyafanyia juhudi.”[1]
Kinachopata kufahamika katika Aayah ni kwamba matendo ya mtu hayamnufaishi mwingine, isipokuwa yale ambayo yeye amesababisha. Baadhi ya wanazuoni wameitumia Aayah hii kuonyesha kuwa hatonufaishwa kabisa na matendo ya mtu mwengine. Hata hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza kwamba kuna baadhi ya matendo yanayomnufaisha maiti baada ya kufa kwake, kukiwemo du´aa na du´aa ya msamaha:
وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ
“Na wale waliokuja baada yao ni wenye kusema: “Mola wetu! Tusamehe sisi na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa imani na wala Usijaalie katika nyoyo zetu mafundo kwa wale walioamini – Mola wetu! Hakika ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu.”[2]
فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ
“Basi jua kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na omba msamaha kwa dhambi zako na za waumini wa kiume na waumini wa kike.”[3]
Hili linawahusu waliokufa pia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewaamrisha waislamu baada ya kumaliza kuzika waseme:
“Muombeeni ndugu yenu msamaha na mtakieni uthabiti; kwani hakika punde tu atahojiwa.”[4]
Kadhalika swadaqah inamfaa maiti. Kuna mtu mmoja alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:
“Hakika mama yangu amefariki na kama angeliweza kuzungumza basi angelitoa swadaqah. Je, nimtolee swadaqah?”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ndio.”[5]
Vivyo hivyo hajj. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Jifanyie hajj mwenyewe, kisha ndio umfanyie hajj Shubrumah.”[6]
Haya ni matendo ya wengine ambayo yanamnufaisha maiti. Vilevile alipokuja mwanamke mmoja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumuuliza kama inafaa kwake kumuhijia mama yake ambaye alikutana na faradhi ya hajj lakini hakuwahi kuhiji, akasema:
“Ndio, muhijie mama yako.”[7]
Kwa hivyo mambo haya – bi maana du´aa, du´aa ya msamaha, swadaqah, hajj na´Umrah – yanamnufaisha maiti na yanaifanya maalum Aayah isemayo:

“… na mtu hatopata [malipo] isipokuwa yale aliyoyafanyia juhudi.”[8]
Kundi lingine likachupa mpaka na kusema kuwa maiti ananufaika na matendo yote. Matokeo yake wanakodi wasomaji wa Qur-aan kuja kuwasomea wafu. Kitendo kama hichi hakimnufaishi maiti wala aliye hai. Kwa sababu msomaji ameshachukua malipo yake juu ya kisomo chake, kwa ajili hiyo hapati thawabu. Isitoshe kitendo hicho kimezuliwa na hakina dalili. Endapo kiwango hicho cha pesa angelitolewa swadaqah maiti, basi kingekuwa kimeafikiana na Sunnah na kingelimfaa maiti. Lakini kwa njia hii ya kizushi hakimnufaishi maiti wala aliye hai. Hii ndio natija ya kuachana na Sunnah.
[1]53:39
[2]59:10
[3]47:19
[4]Abu Daawuud (3221).
[5]al-Bukhaariy (2670) na Muslim (1004).
[6]Abu Daawuud (1811), Ibn Maajah (2903) na Ibn Khuzaymah (3039).
[7]al-Bukhaariy (1852).
[8]53:39
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 216-218
- Imechapishwa: 16/04/2025

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 216-218
Imechapishwa: 16/04/2025
https://firqatunnajia.com/198-matendo-ya-aliye-hai-kwenda-kwa-maiti/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)